Spika Ndugai na Katibu wa Bunge wapelekwe Mahakamani kwa kutoiheshimu Katiba waliyoapa kuitetea

Anzeni kwanza chadema kukataa ruzuku inayotoka kwenye serikali ambayo imeingia kwa uonevu Then ndio mje na ishu ya ndugai
Ruzuku haitoki kwenye serikali haramu Bali inatoka kwenye kodi inayokusanywa toka kwa Watanzania.
 
Kama Chadema walivyojiwekea sheria ndani ya Katiba yao kulinda udhalimu wao eti Mwanachama akienda Mahakamani kukishitaki chama basi moja kwa moja uanachama wake unakuwa umekoma
Ukiwa hutaki kipengele hicho cha katiba basi hujiungi na hicho chama, unaenda TLP au CCM.
Hata FIFA wana kanuni kuwa mambo yao yana taratibu zao kuyatatua, ukienda mahakamani unakuwa umejitoa FIFA
 
Kwa nionavyo..katiba itaendelea kukanyagwa kwa kiwango cha kutisha baada ya kukamilisha 'lile' la kuondoa ukomo wa muda kwa Rais Magufuli.

Ni suala la muda tu kujongea.!
 
Namkumbuka Saddam Hussein, akiwa kizimbani alimuuliza Jaji nani kakupa mamlaka ya kunihoji mie?
Mwisho aliishia kula kitanzi kwa maamuzi ya huyo aliyehoji mamlaka kayatoa wapi!
 
Ujinga mwingine ni pale mtu anapotoka madarakani anatunga kitabu na kuandika maovu na mazuri ya awamu yake, utadhani hakuwepo wakati huo.

Hii ni mbaya sana, pembeni kuna raia wanashangilia na kusema safi, 😖😷!
 
Sasa imekuwa Jambo la kawaida kwa viongozi wa ngazi za juu kuvunja katiba bila ya kuchukuliwa hatua yoyote. Labda swali la kujiuliza ni nani mwenye wajibu wa kuchukua hatua pale viongozi wanapofanya mambo hayo kwa kiburi kilichopindukia. Mtu anasema hadharani kwamba atawalinda wahalifu na hakuna mtu wa kumchukulia hatua. Mbaya zaidi sasa wamejitungia sheria ya kuwalinda na kutoshitakiwa kwa makosa yao bila kujali ukubwa wa kosa. Kwe bunge lilopita ni Ndugai huyuhuyu aliyeruhusu kama siyo kulazimisha Cecil Mwambe sender kuhudhuria vikao vya bunge hata baada ya kutangaza hadharani kuwa amejivua uwanachama wa chama kilichomdhamini. Ubunge wa Zito Kabwe ulikoma na yeye kuacha kuhudhuria kuacha vikao mara baada ya kutangaza kujitoa CHADEMA. Hii ilikuwa enzi ya Makinda. Ndugai ameambiwa na spika mstaafu na aliyeheshimika Msekwa kuhusu ukomo wa ubunge pale mbunge anapokosa udhamini wa chama lakini kwa kiburi ameamua kupuuza tufanyeje?
 
Ivi ndugai, jajo mkuu na magufuli si kwa sasa hawawez kushitakiwa??
 
Fuatilia mambo vizuri. Uamuzi wa kamati ulitolewa taarifa kwa spika na kwa kawaida uamuzi uapotolewa utekelezaji wake unaanza mara moja hadi maamuzi ya ngazi za juu yatakapotolewa. Rejea kesi za Lijualikali na Sugu.
 
Fuatilia mambo vizuri. Uamuzi wa kamati ulitolewa taarifa kwa spika na kwa kawaida uamuzi uapotolewa utekelezaji wake unaanza mara moja hadi maamuzi ya ngazi za juu yatakapotolewa. Rejea kesi za Lijualikali na Sugu.
Kwa mara nyingine nakushukuru sana ingawa tangu mwanzo nilisema "kwa uelewa wangu".Asante muungwana.
 
Hatuendi na katiba, mbona Mwambe alijitoa Chadema akajiunga CCM na akarudishiwa ubunge wake wa Chadema kupitia CCM.
Waliweka sheria inayokataza kushitakiwa hata aistaafu.
 
Nimependa nebula "kinga bandia"
 
Chadema wenyewe wamekaa kimya ww uko kisiju huko unakuwa kimbelembele
 
Nilijua wamepelekwa mahakamani kumbe unatoa pendekezo.
Endelea kutoa mapendekezo
 
Ambae angewapeleka kaamua kuwa mbelgiji bila sababu zozote za msingi
 
Hakuna Jambo rahisi Kama kuwaongoza wafuasi wa chadema,Wana uwezo mdogo sana wa kufikiri,hawana nguvu ya kuhoji,hawajui wanataka nini
Chadema ilitangaza kutoyatambua matokeo yote ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020,Cha kushangaa!!
Madiwani wote wameapa mabarazani
Mbunge wa Nkasi,ameapa bungeni
Chama kinapokea ruzuku inayotokana na matokeo yaliosuswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…