#COVID19 Spika Ndugai, nani alikushauri kufanya haya unayofanya?

Jasusi Mbobezi

Senior Member
Joined
May 17, 2020
Posts
195
Reaction score
851
Ndugu yangu Ndugai alitangaza ratiba mpya ya Bunge (vikao kuanza saa 8 mchana) na jinsi wabunge watakavyokaa wakiwa Bungeni (kutumia kumbi 2), pia alitangaza kuwa wabunge wote wavae barakoa isipokuwa wenye changamoto za kiafya tena kwa kibali maalumu.

Maswali yangu:
1. Kama kweli wawakilishi Hawa wanajali wananchi kwanini ratiba za taasisi nyingine hazijabadilika mf. Shuleni walimu na wanafunzi wanafika mapema asubuhi, wanakaa darasani kwa msongamano, wanatoka saa 9 nanusu mchana, wengine wanaishi huko huko.

Ina maana wabunge walikuwa wanakaa kwa msongamano kuliko shule za kata kiasi kwamba wakaona watumie kumbi 2?

2. Kama wao kweli ni wawakilishi wa wananchi, kwanini hawaishauri Serikali isimamie taasisi kama shule ziwe na shift?

3. AMEKUMBUKA KUPUNGUZA POSHO PIA AU WAMEPUNGUZA MUDA WA KAZI TU?

Hitimisho: wanacho kifanya hawa ndugu zetu ni usanii tu na kujikomba.
 
Inafikirisha!
Kama kuna vitu niliacha kufuatilia basi kimojawapo ni bunge!
Wizi mtupu,wako kwa ajili ya maslahi km wengine tu wanaotafuta mkate wao wa kila siku!

Mungu tu anatusaidia watanzania kwenye kila jambo!
 
Ndugai ameanzisha mfano akiwa kama kiongozi wa mhimili wake, wengine wafuate, japo itakuwa ngumu. Samia huku anasema Corona ipo, kule anakutana na wananchi njiani wasio na tahadhari yoyote wala hana habari.

Viongozi wa chama kimoja, ila wengine wanaelekea kaskazini wengine kusini kwenye jambo moja, hawa watu ndio wanatuongoza kama taifa.
 
Ndugai ni kibaka tu
 
Hapo wamewaiga Kenya tu ili usiku wawe wanapombeka wasiingie na hangover. Aisee Kitwanga ingekuwepo hii yasingemkuta yakumkuta

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani wanapoteza mwingi bungeni ili kupata posho wakati hawana ya kujadili....
 
Lengo hapo ni kuongeza muda wa kikao badala ya wiki 2 watumie wiki 3, kifupi ni kupiga pesa ya umma.
 
Inafikirisha!
Kama kuna vitu niliacha kufuatilia basi kimojawapo ni bunge!
Wizi mtupu,wako kwa ajili ya maslahi km wengine tu wanaotafuta mkate wao wa kila siku!

Mungu tu anatusaidia watanzania kwenye kila jambo!
Wezi wa keki ya taifa
 
Jamaa anajua kabisa mwaka huu hauishi na hatoboi kwahiyo anafanya atakalo
 
Fedha za Corona zitawatesa Sana na hivyi haijulikani itaisha mwaka gani huko kwa mabeberu,watajuta.

Nchi haina janga inalazimisha iwe janga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…