Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta amedai kuwa kuna mtu/watu wamekuwa wakimtumia ujumbe wa vitisho kupitia simu yake ya mkononi. Akizungumza na TBC Taifa, Spika Sitta alidai kuwa ameshatoa taarifa ya jambo hilo polisi kwani hawezi kupuuzia vitisho hivyo ingawa alidai pia kuwa hao ni watu wanaokerwa na utendaji wake mzuri wa kazi.
1. Ni aibu kubwa sana kwa taifa, inapofikia mahali Spika wa bunge, anakuwa reduced to this level yaani ya kulalamika kama sisi wengine wananchi wa kawaida, kwa sababu ungetegemea kiongozi wa nafasi kama yake kua analindwa vizuri sana na system yetu, sasa kama Spika analalamika kua anatishwa, sisi wananchi wa kawaida itakuwaje na hivyo vitisho, maana nilitegemea kwua simu zkae zinakuwa connected na security system kwamba ukimtumia wanaweza kuku-trace within some few minutes wakajua wewe uliyemtumia ni nani, au?
2. Six alikuwa ni mmoja wa the rock wa kundi la Mtandao, the dataz ni aliahidiwa u-Waziri Mkuu, lakini kwenye process za kampeni Lowasssa, akaibuka kuwa the most effective wa kampeni chafu na hivyo kumpiku ukaribu na muungwana na hata kupewa u-PM, ni Lowassa na Rostam ndio walioamua apewe u-Spika, ni Rostam ndiye aliyemuambia achukue fomu ya u-Spika, na ni Rostam ndiye aliyemtuma Amina RIP, kumpelea ujumbe Msekwa kuwa hatakiwi na Mtandao asichukue fomu, lakini Msekwa hakukubali akaishia kuaibika.
3. Six na Mtandao, walitumia mbinu chafu sana kumuondoa Msekwa, kwa kumtumia Mtandao mwingine Marehemu Akukweti, aliyekua naibu wake kwa muda mrefu sana, kwamba aliiba hela nyingi sana kwenye ujenzi wa bunge jipya, ambao the dataz ni kuwa Msekwa, Sumaye na Lukuvi wametengeneza hela nzuri sana na ile kampuni moja ya Ireland.
- My point hapa ni kwamba Six sio mgeni wa michezo michafu ya siasa, wakati anatumia uhuni kumtoa Msekwa, hatukusikia Msekwa akipiga kelele za wolf! wolf! kama anazopiga yeye sasa, wakati akiwatukana sana wagombea wengine behind magazeti yote ya Mtandao kwenye kampoeni za urais wengine hawakupiga kelele kama anazopiga yeye sasa.
4. Sio siri kwamba yeye sasa yuko upande wa pili wa Mtandao, kwa sababu ya kushindwa kuwalinda kama walivyotegemea wakati wanampa ile nafasi, na tayari Mtandao wameshapeleka watu wawili wa kugombea naye ubunge ili wamtoe, pia kule kwa Mwakyembe tayari hawa mafisadi wamesham-recruit dada wa RC Mwakipesile, ili amuondoe Mwakyembe, nako kwa naibu Spika pia wamesha-recruit mtu wao wa kumuondoa, the dataz ni kwamba kuna wabunge 36 ambao Mtandao waliamua kwenye kikao chao cha siri huko Morogoro ambacho kiliongozwa na Nchimbi, kwamba ni lazima waondolewe at any cost Membe pia ni included kwenye hiyo list ya 36, kwa sababu na yeye ni threat kwa urais wa 2015.
5. The dataz ni kwamba katika kikao hicho the mtarajiwa wao Mtandao wa 2010/2015 Mkulu Masha, alionywa vikali sana na wajumbe kwamba hawategemei kuja kua betrayed tena kama Muungwana alivyowafanya sasa, na akithubutu basi yatamkuta makubwa sana.
Six, aaache kupiga kelele za mbweha kila wakati katika kutafuta umaarufu na wananchi, umaarufu na wananchi ambao anautafuta sana kwa sababu za kutaka urais ataupata kwa kuchapa kazi ya wananchi. Kwanza ni lazima tuamini kwamba amejitoa completely na Mtandao, na kwamba sasa tunaweza kumuamini, lakini sio kutuchezea akili na mbinu za kitoto kama this one.