Spika Samuel Sitta adai kutumiwa Ujumbe wa Vitisho

vimada ni asili kwa watanzania haswa wa yale makabila ya asili ya wake wengi, ila kutumia mali ya umma kuhudumia viimada sio maadili. pamoja na yote, spika sita ni spika wa viwango. kabla yake bunge letu lilwahi kuitwa bunge butu' kongoli neno bunge butu kwenye google. sasa bunge lutu sio bunge butu tena.
 

Hilo ni kweli, na ndo maana binafsi naona mafisadi lazima hawako happy naye, kwahiyo lazima wamtishe ili awatii wazidi kutukamua! Walau ukilinganisha na Msekwa six kidogo kafungulia hoja za msingi kabisa kuliko kila kitu ndani ya mbunge kuwa CCM CCM hata mikataba mibovu ina sainiwa watu wazima wanakenua meno tuuu CCM CCM grrrrrrrrrr!!!
 

Pasco,
Bunge letu bado butu. Tusiwe kama watoto wadogo ambao akipewa hata mtumba uliopauka kwake atafurahia kuwa ni nguo mpya. Bunge letu ni mhuri wa raisi na chama chake. Linashughulika labda chini ya 10% ya majukumu yake na ndio maana nchi bado inayumba.
 
Mimi na wasiwasi na kauli za Spika kila baada ya muda kutangaza kutumiwa ujumbe wa vitisho,isije ikawa ni mbinu tu ya kuwa kwenye news asisahaulike na iwe noted huwa inatokea bunge likiwa likizo.
 
Leo ametangaza tena kuwa waliomzushia kashfa ya ufisadi (ile habari ya kutumia vibaya fedha za Bunge) ni maadui wake kisiasa ambao walikuwa na lengo la kumbomoa
 
Leo ametangaza tena kuwa waliomzushia kashfa ya ufisadi (ile habari ya kutumia vibaya fedha za Bunge) ni maadui wake kisiasa ambao walikuwa na lengo la kumbomoa

Ndio zake huyo design kama Mengi vile kula baada ya muda anakuja na madai anatishiwa kuuawa nk the best way to defend is to attack
 

Imetolewa mara ya mwisho: 05.12.2008 0006 EAT

• Polisi wachunguza vitisho kwa vigogo

*Ni Sitta, Mwakyembe, Kilango na Mengi
*Spika: Huu ni uhalifu wa kisiasa, sitishiki

Na Waandishi Wetu
Majira

JESHI la Polisi nchini linafanya upelelezi wa kuwepo madai ya kutishiwa maisha baadhi ya viongozi na wanahabari mashuhuri nchini katika kile kinachoonekana kuwa ni mfululizo wa watu wanaokemea ufisadi nchini kuandamwa, umebaini uchunguzi wa Majira.

Viongozi walioko katika orodha ambayo imelifanya Jeshi hilo kuafanya uchunguzi wa kina ni Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, mbunge wa Same Mashariki (CCM), Bibi Anne Kilango, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya IPP na Bw. Reginald Mengi.

Kwa mujibu wa habari za uhakika kutoka vyanzo vya habari vinavyofahamu kwa kuna upelelezi huo, uchunguzi huo umepata nguvu baada ya Bw. Mengi ambaye juzi alitangaza hadharani kutishiwa kuuawa na Waziri aliyemtaja kuwa kijana na msomi, kuwasilisha rasmi malalamiko polisi na ushahidi wa ujumbe mfupi wa simu ambao pamoja na kutishiwa yeye kupitia ujumbe huo, pia walishiwa kuuawa kwa sumu Spika, Mama Kilango, Dkt. Mwakyembe na Bw. Kubenea.

Bw. Mengi, kwa mujibu wa taarifa za polisi, aliripoti rasmi tishio hilo Septemba 24 mwaka huu na kufungua kesi ya kutishiwa maisha.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu hivyo, ujumbe ambao umewatishia viongozi hao na Bw. Kubenea ambao Mengi aliuwasilisha polisi unasomeka hivi: ''Sitta taarifa ulioitoa haisaidii wewe na wenzio Mengi, Kubenea, Mwakyembe na Kilango mtauawa tu kila kitu kiko katika mstari, (John) Malecela (mbunge wa Mtera CCM) mwambie mkeo (Anne Kilango).

" .....(ujumbe huo unamtaja mfanyabiashara mmoja) alituma vijana wawili UK (Uingereza) kutafuta sumu aina ya RICIN ambayo inaweza kuua ndani ya saa 48, vijana hao waliuawa na wanausalama wa mataifa makubwa duniani kwani walidanganya sumu hiyo ni ya kumuua Balozi wa Taifa moja wakidhani wakisema hivyo watauziwa.''

Majira lilifanikiwa kufanya mahojiano na baadhi ya viongozi waliotajwa kwenye ujumbe huo ambao walithibitisha kupokea vitisho kama hivyo kwa nyakati tofauti.

Spika wa Bunge, Bw. Sitta alisema taarifa za vitisho hivyo zilitolewa kwa viongozi mbalimbali kulingana na misimamo yao katika vita dhidi ya ufisadi nchini.

Alisema Agosti mwaka huu, alitumiwa ujumbe wa aina hiyo akitishiwa maisha yake na alilazimika kuwasiliana na walinzi wake ambao walikwenda kutoa taarifa za vitisho hivyo Polisi.

"Simu tunazopigiwa na ujumbe tunaotumiwa katika simu zetu ni uhalifu wa kisiasa hivyo ni wajibu wa Jeshi la Polisi kuchunguza taarifa hizi kwa mtu yeyote anayetishiwa maisha yake," alisema Bw. Sitta.

Bw. Sitta alisema, vitisho alivyowahi kutumiwa havimpi wasiwasi kama inavyochukuliwa na wahusika wa uhalifu huo, bali ataendelea kusimama katika misingi ya kazi yake kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Naye Dkt. Mwakyembe alipoulizwa kwa njia ya simu jana alisema msimamo alionao katika vita dhidi ya vitendo vya ufisadi nchini, umemjengea uadui na kupata vitisho tofauti kwa njia ya simu na ujumbe mfupi wa maandishi.

Alisema vitisho vya aina hiyo, pia vilitolewa kwa viongozi wengine ambao walionesha misimamo yao katika suala hilo lakini vitisho hivyo, sio kigezo cha kuwafanya viongozi hao kushindwa kutetea maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Alipotakiwa kuelezea baadhi ya maneno yaliyokuwa katika ujumbe ambao Bw. Mengi amelazimika kuuwasilisha polisi, Dkt. Mwakyembe alisema, vitisho hivyo vilitolewa muda mrefu na kusisitiza kuwa polisi wanataarifa juu ya vitisho hivyo.
 
Polisi fanyeni kazi acheni siasa , mkiamua kutumia elimu yenu mtawapata, na hawa wanaopigana na ufisadi kumbuka wanawasaidia nyie..
 

Hi huyu alipewa siku ngapi athibitishe kauli yake la sivyo hatua za kisheria zingechukuliwa dhidi yake?
 
Yaani haya ni mambo ya ajabu kabisa!

Labda kundi hilo lingine la 2010-2015 litakuja na "elements" za change walau wakulima wafaidike na kilimo chao la jembe la mkono.

Hili suala la simu za viongozi wa serikali kuzagaa mitaani ni jambo la kuzingatiwa kwani unaposhirikisha masuala kama ufisadi, uhawala na uhuni mwingine basi namba ya simu itazagaa tu upende usipende.

Lakini "hold on", Samwel Sita sasa apumzike.
 

Kama kawaida yako wewe kila kitu unajua na unajitahidi sana kuonesha umma wa JF kuwa ni mtu wa dataz na kujuana na viongozi. Nikujaribu kuangalia motive yako humu sioni kama ni independent kama za wakuu wengi humu ila naona either unatumika au unataka kutumika baadaye.

Mimi siyo mtu wa kukueleza kitu utakachotaka kusikia tu no!! nitakueleza hata yale usiyotaka kusikia. Kumbuka pia kuwa watu wanabadilika na kuacha uovu na mmojawapo ni Sita, sasa kama hiyo utaki ni wewe mwenyewe na siyo kutaka kila mtu aamini hivyo. oooh mtandao sasa asingejiunga na mtandao angepataje uspika na khali mtandao walitawala kila kit, hiyo ilikuwa ndiyo njia pekee ya kupata madaraka na sasa anataka kuitumikia nchi yake. Huyo ni good guy.

haya ni maoni yangu na nategemea utayafanyia kzai bila kutumiana vijembe humu.

Mungu akubariki na akugeuze na wewe kama bado haujageuka
 
Usimpake mafuta ya uturi kama unaamua kuwa sheikh ukubali kuvaa kanzu muda wote kama utataka kuvaa bukta ushekhe utakushina hivyo basi viwango kwa kiongozi safi pamoja na kutokuwa mzinzi.
 
1.
- Kwanza samahani kwa kukukwaza kwenye ile topic ya rais na kutojiamini maana najua ndiko hasira zako zilikotokea.

- Either nina dataz au sina, either ninajua viongozi au siwajui chagua moja na uweke hapa, tuendelee na mjdala kama unavyoutaka.

- Kutumika hapana nimeshapewa sana hizo nafasi na unajua sana hilo nikazikataa, sasa kama wewe unatumika hapa sio lazima na sisi wote tuwe, si unajua kuwa msema njia hua lazima aliipitia, au? Na what is your point anyways maana siioni?


2.
Mimi siyo mtu wa kukueleza kitu utakachotaka kusikia tu no!! nitakueleza hata yale usiyotaka kusikia.

- Who are you and where? Listening to you since when? Yaani uantokea wapi na hizi nyepesi nyepesi?

3.
Kumbuka pia kuwa watu wanabadilika na kuacha uovu na mmojawapo ni Sita, sasa kama hiyo utaki ni wewe mwenyewe na siyo kutaka kila mtu aamini hivyo.

- Sita sio tu alikuwa mtandao, bali aliahidiwa uwaziri mkuu nilisema toka BCS, lakini lowassa akamzidi kete, yes alikua mtandao tena damu, ndio maana hata mke wake alipewa uwaziri, lakini sasa amebadilika na kuwa mpiganaji na nimesema hayo mapema sana, now what is your problem hapa?

4.
- Irrelevant, mbona unaweka mkwara wakati ni wewe mwenyewe ndiye uliyeanza kutuma vijembe? Nikutumie vijembe for what?

5.
Mungu akubariki na akugeuze na wewe kama bado haujageuka

- Kama kweli huyu Mungu wako anawageuza wananchi kutokana na mawazo yao kwenye forum, basi nafikiri kila atakayesoma hapa ataamua kwamba ni nani hasa kati yetu anayeihatji kugeuzwa as of your claim, maana hii forum ninaiaminia sana kwa kusoma between the lines!

Good try, thanxs!
 
Mkuu ES, nakuomba sana mkuu I get ur points on their merits but Tanzania is fighting a big war against ufisadi na mtandao, so we need to see things in there totality.

Spika sasa hivi anaprotect wabunge wengi mno some ambao without saying we need them to be protected. Sasa tutakapoanza kumrushia tena vijembe huyu huyu Spika ambae wote tunamtegemea kulipa bunge meno ya kutetea wananchi wa Tanzania tutakuwa tunacheza Checkers humu ndani na sio chess.

At the same time Masha hana interest za wananchi sababu anatetea mafisadi kwa nguvu zote, sasa hata kama mtu unamjua au sababu ni kijana mwenzetu kwa kutowatetea wananchi anakuwa amefanya SIN kubwa mno ambayo inamdisqualify kutetewa kwenye lolote kutoka kwa wapenzi wa nchi.

Ni hayo tu Mkuu.
 
Shalom,
Mkuu kama una hoja ziweke haya maswala la kushambulia mtu kabla hujaandika hoja yako unaleta picha mbaya..
na ajabu ni kwamba unakubaliana na yote aliyoandika isipokuwa unachoongezea ni msisitizo tu kuwa Sita ni good guy!..sidhani kama FMES kasema huyu sio good guy isipokuwa kama malalamiko yake anayapeleka kwa wananchi tuna kila haki ya ku qustion nafasi yake ktk Mtandao ambao ndio wamemweka madarakani. Na zaidi ya yote kaonyesha hata yeye Six kuwepo ktk hatari ya kuondolewaktk kiti chake, hapa katupa sura mbili za sarafu..
FMES kaeleza vizuri na katufungua macho wengine hata wahusika wake.. kama unapingana na dataz hizo mwaga manyanga mkuu, hakuna mtu anataka kufahamu jitihada za FMES..
Tumeyaona mengi yaliyopitishwa ama kuzuiwa na Six, kiasi kwamba tunashindwa kuelewa kasimama upande gani!
 

1. Mkuu kwenye hoja ya Spika tupo ukurasa mmoja labda tu hatukuelewana lugha.

2. Kama kuna ukweli wa kisheria juu ya maksoa ya waziri wa ndani, yawekwe wazi ili achukuliwe hatua za kisheria, tuachane na habari za mtaani, huu ni wakati wa uwazi na ukweli, hakuna kufichana tena.

Otherwise, siku zote you have my respect najua wewe sio mkurupukaji, na nimekusikia loud and clear! Mengi apunguze mambo ya kurukia vimwana wadogo maana haya ndio matokeo yake.
 

utendaji upi mzuri wa kazi alio nao Sitta?to me he is just an opportunist hana lolote,anajidai kupinga mafisadi mwenyewe anakaa nyumba ya $8000 kwa mwezi!!lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…