Spika Samweli Sitta amepoteza shilingi

Spika Samweli Sitta amepoteza shilingi

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,750
Unajua Sita alikuwa hana hela akaenda kukopa kwa watu wawili ,akihitajia shilingi mia tu ,hivyo akakopa kwa kila mmoja shilingi 50 .akatimiza mia.

Akaelekea dukani ,akanunua begi la shilingi mia ,mwenye duka akampunguzia bei kwa kumrudishia shilingi tatu, Mheshimiwa Sita kwa vile ni spika akaona akapunguze deni, akawarudishia wale jamaa shilingi mbili na moja akaona abakie nayo mwenyewe.

Sasa kindende wakati muheshimiwa Sita akirudi akaangalia akafikiria deni lilobaki kwa wale jamaa aliowakopa ni shilingi 49 kwa kila mmoja ,akazijumlisha akapata 98 akongezea na ile shilingi yake zikawa shilingi 99 ,Sita akili ikamvurugika anaona mbona ni 99 shilingi moja imekwenda wapi ? Mbona akidi haikutimia?

Wakati tokea walipoondoka Ukawa alikuwa na idadi kamili ya wajumbe anaowahitaji kwa kupata 2/3 ,Mheshimiwa sasa anahangaika kuitafuta shilingi.
 
mfano murua kabisa kwa mtu mwenye kichwa kizito kama sita
 
Unamaana Sitta ( Kamati za Bunge Wenyekiti toka Upinzani) = Ndugu Gai + Covid - 19 Minus Covid -19. Kweli hesabu za Sitta Hazisomi..
 
Back
Top Bottom