saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Hali ya mafuta ni mbaya ambapo leo watanzania wenzetu wa Kyerwa Ruberwa Mkoa wa Kagera wanauziwa mafuta ya Petroli kwa Tsh 3,647 kwa lita huku wale wa Ukerewe Mkoa Mwanza wakiuziwa lita moja kwa Tsh 3,619 kwa mujibu wa Tangazo la EWURA.
Mjadala huu umeitikisa nchi tangu bei hiyo mpya itangazwe na EWURA usiku wa kuamkia leo huku watanzania wengi wakimtupia lawama kubwa Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kwa kitendo cha kuzima hoja hiyo ilipoibuliwa bungeni kwa kile kinachodaiwa kulinda kibarua chake.
Wengi wanamtuhumu Dk. Tulia kwamba ndiye amelitumbukiza Taifa kwenye mgogoro huu mkubwa kutokana na kitendo chake cha kukataa ushauri uliotolewa bungeni na Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu kuhusu mchezo mchafu unaofanyika kwenye mfumo wa uagizaji wa mafuta.
"Kuna tatizo kubwa la bei ya mafuta katika nchi hii ambalo linaendelea kwa kasi kubwa na kutokana na hali hiyo ni kwamba mafuta yaliyoagizwa katika tenda za Tarehe 28/3/2022 tenda ile ilichezewa asubuhi ilitoka tenda nyingine, jioni ilitoka tenda nyingine, matokeo yake Mh Spika ni kwamba......" kabla hajamalizia Spika akamzuia kuendelea kusema.