Samson Kwayu
Member
- Jun 9, 2022
- 19
- 94
Leo asubuhi tumeshuhudia jinsi spika wa bunge Dokta Tulia akihaha kuhalalisha kuwa kikanuni akidi (idadi) ya wabunge imetimia na mjadala wa bajeti ya wizara ya nishati itaendelea tu japo kuna wabunge zaidi ya 200 wamesusia mjadala wa wizara ya nishati leo asubuhi.
Dr. James Andilile ni mume wa Spika Tulia na picha hii ilipigwa siku moja kabla ya bajeti wakati wizara hii ikifanya bonanza la kugawa mitungi ya gesi ambayo imetafsiriwa kama ni rushwa na Spika akatoa ufafanuzi jana kuwa hiyo siyo rushwa ni jambo la kawaida sana na liko kwenye bajeti ya wizara ya 2022/23. Japo tumetafuta sana fungu hili la kununua mitungi na kuigawa hatujaona kwenye bajeti aliyosema Spika Tulia.
Kwa kuwa mume wa Spika bwana Dr. James Andilile ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ambapo waziri January Makamba anaisimamia EWURA akiwemo bwana James kwa vyovyote vile simuoni Spika Tulia akijizuia kupendelea na kutetea wizara anayotoka mumewe pale inaposhughulikiwa kwa michango ya wabunge au ukosoaji nje ya bunge.
Hili ni tatizo la kimaadili na kiuadilifu na kwa kutambua hilo nilitegemea Spika Tulia akae pembeni wakati wa mjadala huu ili kuondoa maneno yanayozagaa kuwa amekuwa matari wa mbele kutetea rushwa na uvunjwaji wa kanuni kwa kuwa wizara hii inamhusu mume wake.
View attachment 2642564