Spika Tulia akemea Wabunge wanaotangatanga na kupiga kelele wakati Bunge likiendelea

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Spika wa Bunge, Tulia Ackson ametoa onyo kwa Wabunge ambao hawafuati utaratibu wanapokuwa Bungeni ikiwemo kupiga kelele na kuzungukazunguka ndani ya Bunge pasipo kufuatilia kinachoendelea.

“Tufuate kanuni zetu na utaratibu humu ndani ikiwa pamoja na kanuni ya 73 inayozungumzia staha ndani ya Bunge, wapo Wabunge ambao siku nzima anazunguka kiti kimoja kwenda kingine, hata akiambia jambo gani limejadiliwa hiyo siku, hajamsikia mchangiaji hata mmoja.

“Kanuni zipo wazi kutangatanga ndani ya Bunge bila sababu hairuhusiwi, tulizingatie,” - Spika Tulia, leo Mei 23, 2022
 
Tulisema wabunge wa upinzani ni wazururaji na waleta fujo bungeni na tukaweka mkakati tuwe na wabunge wote wa kwetu, sasa kulikoni tena.
 
Kwanza hakuna bunge hapo kuna genge la matapeli tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…