Spika Tulia amuonya Naibu Waziri Katambi kutotumia lugha zisizofaa mfano "waliokosa mikopo ni Wakenya"

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Spika Tulia amemtaka Naibu waziri Katambi kujibu upya swali la Mbunge wa Chadema Mh Sophia Mwakagenda.

Katambi alisema waliokosa mikopo ni Wakenya.

Tulia amesema kauli ya Katambi imezua tafrani kwa vijana nchini hivyo amemtaka Naibu waziri kuwa Makini na kauli zake

Chanzo: Channel ten

Kuhusu Kauli ya Katambi, Soma > Waziri Katambi: Vijana ambao hawajapata mikopo ya Halmashauri pengine ni Wakenya
 
Spika usimguse huyu, alipo kawekwa na wakubwa !! kama walivyo wale waasi 19.
 
Huyo Katambi hata sifa ya uongozi hana nashangaa anakuwaje naibu waziri ndo Mana nchi haisongi mbele kwa aina hii ya viongozi.
.Katambi
.Mwiguli
.Nape
.J.Makamba
.Kijaji
.Mavunde
.Mhagama
.Mashimba
.Gwajima
.Umy Mwalimu

Hawa viongozi hawana ubunifu wowote kiutendaji kazi yao ni kulopoka tu ili waonekane wanafanya kazi lakini kiuhalisia hawana kitu Cha kudeliver .Na ajabu Hawa ndo Mama Samia anawategemea wafanye maajabu .
 
Huyo dogo ana maneno ya shombo sana, simkubali hata kiduchu
 
Chadema ina mbunge mmoja tu bungeni kutoka jimbo la Nkasi.

Pili huyo Katambi alishajiita karai kwahiyo huna sababu ya kushangaa atakachoropoka.

Aliyempa ubunge tayari ameshatwaliwa kuzimu kwahiyo huyu 2025 atarudi mtaani iliapate taste ya maisha, kile kiinuwa mgongo atakitumia kuhonga wajumbe wa ccm lakini hawatomchaguwa, Shinyanga mjini upande wa ccm mtu wao ni Masele na ndio walimpigia kura yule mungu wa chato akamkata jina akalipachika hiki kalai lake lisilo na akili kichwani.
 
Mbona Ridhiwani hujamtaja?
Au yeye ni kiongozi makini?
 
Zaa zimebadilika, tukiandamana humu mtandaoni tu jamaa anaweza kung'oka!
Huyu amebakizwa tu kwa sababu maalum isionekane kuna mkakati maalum wa kuwafagia Sukuma gang, lakini ni swala la muda akiweza kusurvive hadi 2025 wajumbe watapiga spana wenyewe, hawezi kushindana na Masele kwenye kura za maoni, huo ni ubunge wa kupewa tu na 2025 wenye chama chao wanachukuwa ubunge wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…