Spika usiruhusu wabunge waongo waongo kuchochea chuki, Mbowe alisema biashara zake zimefungwa na TRA

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Natoa tu ushauri kwa kiti cha Spika kwamba siyo vema wala haki kuruhusu wabunge kuchochea chuki na fitna kwa jamii tena kwa watu ambao hawako bungeni.

Nilivyomsikia Mbowe ni kwamba biashara zake zimefungwa na TRA baada ya kushindwa kulipa kodi ya tsh 2 bilioni ambayo anaipinga.

Mbowe aliongea kupitia press na wananchi wengi walimsikia.

Sasa anapoibuka mbunge Ngonyani na kumshushia tuhuma Mbowe na familia yake na kiti kinakaa kimya hii si haki.

Kazi Iendelee
 
Bado wanaendelea kudemka hao jamaa mjengoni wakumbuke mama kawakataza.
 
Naona MATAGA mmerudi kwenye uhalisia bila kukumbatia uongo na mapambio kwa mfalme aliyefukiwa
 
Wabunge wasiojua majukumu yao hawa.
Swala la kujibiwa na Serikali(TRA),yeye mbunge anajifanya ndio msemaji.
 
Haya ndo madhara ya kuwa na watu wanaojua kusoma na kuandika tu. Baadhi ya wabunge ni wapuuzi mno. Huyu ngoyani anataka bunge limfikishe kileleni
 
Natoa tu ushauri kwa kiti cha Spika kwamba siyo vema wala haki kuruhusu wabunge kuchochea chuki na fitna kwa jamii tena kwa watu ambao hawako bungeni.

Nilivyomsikia Mbowe ni kwamba biashara zake zimefungwa na TRA baada ya kushindwa kulipa kodi ya tsh 2 bilioni ambayo anaipinga.

Mbowe aliongea kupitia press na wananchi wengi walimsikia.

Sasa anapoibuka mbunge Ngonyani na kumshushia tuhuma Mbowe na familia yake na kiti kinakaa kimya hii si haki.

Kazi Iendelee
Kinachoniuma zaidi yule mama na yeye anapokea 11M+
 
Back
Top Bottom