Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aagiza Kamati iwaite Wakurugenzi wa NSSF na PSSSF Bungeni kueleza kuhusu michango ya Wanufaika

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aagiza Kamati iwaite Wakurugenzi wa NSSF na PSSSF Bungeni kueleza kuhusu michango ya Wanufaika

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameelekeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Jamii kuwaita na kuwahoji wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi za jamii nchini kuhusu madai ya kuwataka wanufaika, kutakiwa kulipa fedha za michango ambazo waajiri wao hawakuilipa mifuko hiyo, ili waweze kupatiwa mafao yao.

Spika Tulia ametoa maagizo hayo Jumanne, Juni 4, 2024 bungeni jijini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kutokana na mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko.

Matiko ameomba mwongozo huo kutokana na swali la Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kasinge aliyehoji changamoto ya baadhi ya waajiri kutolipa michango ya watumishi wao na kupelekea mifuko ya hifadhi kuwataka wahusika wenyewe kuchangia kuziba mapengo.
 
Back
Top Bottom