Eti nini?Wanaendelea kuuhalalisha wizi uendelee, kwamba si Jambo la kushtua hilo.
Kama unaona ni vibaya sasa nenda huko upinzani...tuachie CCM yetu. Pesa hipo nyingi nchi hiiSpika amepotoka CAG anakagua fedha za umma.
Bunge ni kikao cha wananchi na wananchi ndio waajiri wakuu wa watendaji wa Serikali.
Hivyo wanayo haki za msingi kupatiwa majibu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
Hakuna Sheria iliyo juu ya haki hii ya msingi ya wananchi kufahamishwa kuhusiana na utendaji wa Serikali.
SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati wa Mkutano wa Bajeti unaoendelea na kwamba Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na Mbunge kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu Mkutano wa sasa wa Bunge ni wa Bajeti na si kujadili ripoti hiyo.
Pesa nyingi kiasi hicho zilizofisadiwa wahusika wake ni wengi sana na wengine hawagusiki! Ukilazimisha unakwenda na maji!! Keshaona kwa mbali kuwa ni maji marefu au kawekwa kikao na kuambiwa Tulia TULIA kama lilivyo jina lako. Huko mwezi wa tisa wakubwa watakuwa wamesawazisha mambo na mhemuko wa wananchi kuhusu ufisadi huu utakuwa umepungua sana!! Wewe ukiona Mwigullu Nchemba alipata ujasiri wa kumhusisha Rais ujue kuna kitu kizito hapo!!!SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati wa Mkutano wa Bajeti unaoendelea na kwamba Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na Mbunge kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu Mkutano wa sasa wa Bunge ni wa Bajeti na si kujadili ripoti hiyo.