peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Kwa Hali hii, tutarajie nini? Tumepigwa na kitu kizito!
Misri wanakuja nchini kuwekeza Kwa Kasi kubwa.
Hii Ke tunaowaamini, tunauzwa mchana peupe.
==========
Mhe. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) tarehe 22/5/2024 alianza ziara yake ya siku 3 nchini Misri kufuatia mwaliko wa Bunge la Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ambapo alitembelea Bunge la Misri na baadae kufanya Mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Hanafi Gebali.
Wakati wa mazungumzo hayo, Mhe. Hanafi, Spika wa Bunge la Misri alieleza kuwa Bunge la Misri ni Kongwe tokea 1866 lilipoanzishwa na limekuwa na ushirikiano wa karibu na Umoja wa Mabunge Duniani kutokana na kutambua umuhimu wake na majukumu yake katika kuyaunganisha Mabunge Duniani kujadili mambo yenye maslahi ya pamoja duniani kote.
Aidha, kwa upande wa mahusiano na Tanzania, Misri na Tanzania zimekuwa na mahusiano ya muda mrefu tokea enzi za waasisi wa nchi mbili rafiki, Mhe. Marehemu Gamal Abdelnasser wa Misri na marehemu J.K. Nyerere wa Tanzania ambao walishirikiana katika harakati za ukombozi wa nchi mbalimbali Barani Afrika.
Pia, Misri imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kiuchumi katika sekta mbali mbali ikiwemo Nishati, Kilimo, ujenzi na miundombinu.
Aidha, Misri na Tanzania zimekuwa zikishirikiana baina ya nchi na nchi, bali pia zinashirikiana katika ngazi ya Kikanda kupitia Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa kuunga mkono masuala muhimu yenye maslahi ya pamoja.
Hivyo, Misri imemuomba Dkt Tulia Ackson, kwa nafasi yake kama Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, na Spika wa Bunge la Tanzania, nchi yenye ushawishi mkubwa Kimataifa, kumuunga mkono mgombea wa Misri katika nafasi ya mjumbe wa Kamati Tendaji ya UNESCO.
Nae, Dkt. Tulia Ackson, alimshukuru mwenyeji wake na Serikali ya Misri kwa mapokezi mazuri na ukarimu wa hali ya aliopewa yeye na ujumbe aliofuatana nao.
Aidha, aliipongeza Serikali ya Misri kwa jitihada kubwa inazozichukua katika usuluhishi wa migogoro inayojitokeza Barani Afrika na Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na Libya, Sudan, Ethiopia na hivi karibuni Israel na Palestina.
Vilevile alipongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya Misri na Tanzania kidiplomasia na kiuchumi ambapo viongozi wakuu wamekuwa wakitembeleana na kushauriana katika mambo mbali mbali.
Mhe. Spika alipongeza jitihada za Serikali ya Misri kuunga mkono juhudi za maendeleo za nchi nyengine za Afrika ikiwemo Tanzania kwa ujenzi ws Bwawa la Mw. J . K. Nyerere kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa ajili ya kuchochea uwekezaji, viwanda, kilimo cha umwagiliaji maji pamoja na biashara.
Aidha, alisisitiza haja ya kutanua zaidi ushirikiano katika uwekezaji katika mito na maziwa nchini Tanzania pamoja na kuanzisha jukwaa la ushirikiano baina ya Wabunge wa Tanzania na Wabunge wa Misri ili kutanua wigo wa kujifunza, kujenga uzoefu na kubadilishana utaalamu miongoni mwa nchi hizi mbili.
Mhe. Spika na ujumbe wake waliwasili Misri jioni ya tarehe 21 Mei, 2024 ambapo amepangiwa kukutana na Spika wa Bunge la Misri, Waziri Mkuu wa Misri Mhe. Moustafa Madbouli, na kutembelea Pyramids za Giza, Makumbusho ya utamaduni na makumbusho kuu ya Misri.
Ziara itakamikika kwa kutembelea Kanisa la Orthodox la Saint Mary eneo la Maadi na Coptic Museum tarehe 24 Mei, 2024 ambapo usiku ataondoka nchini Misri kurejea Tanzania kwa kupitia Dubai.
Ziara hii ni kielelezo cha undugu na urafiki wa muda mrefu uliopo baina ya Misri na Tanzania lengo ni kuimarisha zaidi ushirikiano huo kupitia Mabunge ya nchi hizi mbili, Misri na Tanzania, kwa upande mmoja na Umoja wa Mabunge Duniani kwa upande mwengine, ambapo Mhe. Tulia Ackson, ameahidi kutoa kila ushirikiano kuisaidia Ofisi ndogo ya Umoja wa Mabunge Duniani iliopo nchini Misri kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.
Bunge