nameless girl
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 4,195
- 2,678
Doctors wote, heshima kwenu wakubwa.
Mimi naomba kufahamu mtu aliyezaliwa na spinal bifida, nini hasa uwa ni chanzo cha tatizo hili. Na mtu mwenye tatizo hili anaathirika vipi kiafya? Je hii uwa ni tatizo la kurithi?
Naomba mwenye uelewa anipe elimu please.
Doctors wote, heshima kwenu wakubwa.
Mimi naomba kufahamu mtu aliyezaliwa na spinal bifida, nini hasa uwa ni chanzo cha tatizo hili. Na mtu mwenye tatizo hili anaathirika vipi kiafya? Je hii uwa ni tatizo la kurithi?
Naomba mwenye uelewa anipe elimu please.
Hii mara nyingi inakuwa congenital abnormality ambayo mtoto anazaliwa na tundu katika uti wake wa mgongo kitaalamu inaitwa spinal bifida.
Tundu hili unaweza kuliona kirahisi ambapo linaitwa ovat bifida.
Tundu hili pia unaweza usilione kirahisi mpaka utakapo palpate katika eneo hilo au kuligusa ndipo utahisi uwepo wa shimo hilo ambapo tunaiita occult bifida.
Hii ni defect inayotokea wakati wa Organogenesis angali foetus ikiwa katika womb ya mama.
Pia infections e.g TORCHERS are known to be the cause.
Madhara ni kwamba
1 .mtoto anakuwa liable kupata infections kirahisi kutokana na uwazi huo.
2.mtoto anaweza kupata abdominal dysfunction due to nerve injury around the affected sitea.
3.mtoto anaweza kupata matatizo ya mkojo na uzazi kiujumla.
Just a summary, wengine wanaweza kuongeza au kupunguza
Pamoja na yale chakii aliyoeleza.
Spina bifida, ni mjumuisho wa aina ya matatizo yanayotokea katika sehemu ya uti wa mgongo yaani neva za fahamu, mifupa, nyama n.k.
Wakati wa ujauzito, wiki za awali mwili wa binadamu anayeendelea kukua tumboni hutegemea lishe(chakula na madini) mojawapo ni yale yenye kuhusika na utengenezaji wa hivyo tukivyosema hapo juu.
Sasa ukosefu wa madini haya/supplements huweza kusababisha magonjwa ikiwepo tatizo ulilouliza. Ndiyo maana wakti wa ujauzito hasa tunashauri pale mwanamke anapojitamvua ni mjamzito kuanza kliniki ya ujauzito mara moja. Huko hupewa baafhi ya Supplements na dawa kukinga magonjwa mbalimbali pamoja na madhara yanayoweza kujitokeza hapo baadaye. mf. Folic acid"vidonge vya njano".
Pia,matatizo haya yameonekana sehemu nyingi ambapo kuwekuwa na mionzi na heavy metals.Mf. takribani watoto wote wenye matatizo hayo hutokea sehemu zilizo na migodi, au kusafiri/kuwa maeneo ya migodi wakati wa ujauzito.