ukimuomba mungu kwa imani,matumaini na maleongo anakupatia fasta.lakini ili uwe tayari kupokea nilazima ukubali kutoa,namaanisha inabidi uvunje ukuta uliojiwekea baina yako na mungu nao ni dhambi hata zile za mauti.mfano wewe ni mzulumati au unafanya ngono ovyoovyo kwa kuvunja amri za mungu na unamuomba mungu akufanye ufanikiwe katika biashara yako;ndugu hapo mungu atakuwekea kizuizi kwa sababu anataka kukuokoa na kwa kawaida mungu hutumia njia ngumu na zisizo za kifikirika ili kukuokoa.Lakini unaweza kusali kwa imani pamoja na yote na ukaishi maisha kamili ya kiroho pasi na dhambi za mauti(namaanisha zile za kuvunja amri za mungu) lakini mungu anachelewa kukujibu,hapo mungu anapima uvumilivu,matumaini na imani yako na huenda anataka kukuokoa na kiti au jambo fulani.Lakini kamwe haiwezekani ukaomba alafu ukakaa tu kama kabeji inasubiri mvua ichipue vizuri, ni lazima upige kazi,utafuta njia thabiti na namna mbalimbali za kufikia ombi lako. "yesu kristo alioneshwa mateso atakayopitia na mungu baba yake akatokwa na jasho la damu na kuogopa sana lakini ilikuwa haina budi alikubali na akasema kama kikombe hicho cha mateso hakiwezi kumuepuka basi mapenzi ya mungu yatimizwe" na kweli wayahudi walimpa kibano wakamuuwa pale kwenye mti wa msalaba ambapo kifo kile kilikuwa kinatafsiriwa ni cha laana na wayahudi. karibu kanisa katoliki parokia au kigango chochote kilicho karibu yako mtafute katekista/mwalimu wa kanisa au watumishi wengineo/waamini ili usali na ufundishwe sala.