Msaada please namna ya kupika cake!!
Keki zipo za aina nyingi, next time fafanua aina ya keki unayotaka tafadhali.
Keki iliyo rahisi ni hii
Spong Cake
Maitaji/Vifaa
EGGS .............................. 5
SUGAR ............................ 1 kikombe cha robo lita
Siagi................................¼ Kg
Vanilla................................ Vijiko 2 vya chai
Unga wa Ngano.................. vijiko vya chakula10
Barking Powder................... vijiko vya chai 2
Zabibu kavu......................... ½ kikombe cha robo lita (si lazima)
Jinsi ya kutayarisha:
Tia mayai na sukari kwenye blender saga mpaka iwe nyeupe (laini) kisha tia siagi (i.e Tan Bond or Blue Band) endelea kusaga mpaka iwe laini kabisa tia zabibu ¼ cup, baking powder, vanilla,and cocoa (Ukipenda) endelea kusaga halafu mwisho utatia unga vijiko 5 utamalizia kuchanganya kwenye bakuli sababu blender halitosaga kisha tia kwenye trea ya kuokea na juu utatia zabibu Kisha utaoka.
Jinsi ya kujuwa kama keki ipo tayari ni kuingiza kijiti kwenye keki na kikitoka na mchanganyiko unao nata ujuwe bado, ila kikitoka kikavu basi keki yako ipo tayari, pia hata rangi ya nje utaiona imebadirika.
Enjoy.