Mziray anajivunia lile kombe la challenge mwaka 1994, wakati n Mkwasa ambaye alifanya mambo. Fuatilia: kila Mziray alipochaguliwa kufundisha timu ya taifa, lazima aliwaita "MAKOCHA", Mkwasa au Kibadeni kama si Sunday Kayuni!
Jana (09/11/2009), kupitia kituo cha redio cha Magic FM, Mziray alitukana sana! Alidiriki kuziita kampuni zinazoifadhili Taifa Stars (Serengeti Breweries, NMB, nk.), eti ni "vijikampuni", akadiriki hata kuwaita wachezaji wa T. Stars ni "wachezaji uchwara"; huyu anayejiita msomi anavurumisha mitusi LIVE kwenye redio, halafu bado watangazaji wa hicho kituo (Cyprian Musiba, Clifford Ndimbo na Said Kilumanga), wanashabikia ujinga badala hata ya ku-hariri mahojiano yale ( hawakuelewa, hata wao walitukanwa)! Hivi watanzania tunataka nini hasa? Ni kweli Maximo kumpanga Ali Mustapha akae golini, hilo lilikuwa kosa kubwa (maana hajacheza mechi yoyote tangu msimu huu wa ligi umeanza). Lakini je, tulitegemea tungeweza kuwafunga wamisri walio na Aboutreika, Amri Zakhi, Barakat na wengineo??
Ni kutokana na chuki zisizo na msingi ndo maana jamaa wanachukia kukosa ulaji kama wakati ule.
Maoni yangu ni kuwa timu iliyopo itunzwe, kama ni mabadiliko ya wachezaji yawe machache kulingana na mahitaji! Vinginevyo tuendeleze vijana ili miaka michache ijayo tuwe na timu nzuri na imara! Siyo tukishinda; Maximo Hoyeee, tukifungwa Maximo Hovyooo!
Tusipochafuka tutajifunzaje???????