SportPesa Super Cup: Singida United yawa mshindi wa 3! Simba yapigwa 2-0 na Gor Mahia, yawa mshindi wa 2

SportPesa Super Cup: Singida United yawa mshindi wa 3! Simba yapigwa 2-0 na Gor Mahia, yawa mshindi wa 2

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Klabu ya Singida United kutoka Tanzania imefanikiwa kuwa mshindi wa tatu katika Michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kakamega HomeBoys kwa penati

IMG_20180610_141647.jpg

Singida imeishinda Kakamega kwa penati 4-1, walipigiana penati baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika wakiwa wamefungana goli 1-1

Kakamega ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Wickleaf Opondo mnamo dakika ya 4. Lakini Singida waliweza kusawazisha kupitia kwa Danny Lyanga dakika ya 61

Katika mchezo huo Nahodha wa Singida Deus Kaseke ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi ya mshindi wa tatu akichaguliwa na jopo la makocha kutoka Everton

IMG_20180610_141701.jpg

Mikwaju ya penati ya Singida United imefungwa na Deus Kaseke, Miraji Adam, Danny Lyanga na Shafiq Batambuze
========

Michuano hiyo ambayo inamalizika leo, itamalizika baada ya mechi ya fainali kati ya Simba SC(Tanzania) na Gor Mahia(Kenya) kuchezwa. Mechi hii inaanza majira ya saa 9:00 alasiri

IMG_20180610_142213.jpg

Mpira umeanza Katika Dimba la Afraha

5' Gooooooal
Meddie Kagere anaiandikia Gor Mahia bao la kuongoza baada ya shuti lake kumshinda golikipa Aishi Manula

Gor 1-0 Simba

IMG_20180610_155020.jpg

56' Gooooooal
Jacques Tuyisenge anaiandikia Gor Mahia bao la pili

Gor 2-0 Simba

Video

 
timu za afrika kwanini ni shida sana kufungana mabao mengi kwenye dk 90?
 
naweza kutazama hii mechi ya simba online? naombeni link au channel ya kutazamia. Asante
 
naweza kutazama hii mechi ya simba online? naombeni link au channel ya kutazamia. Asante
KAMA UNA SIMU JANJA PAKUA APP YA AZAM AU STARTIMES KUTOKA APP STORE AU PLAYSTORE KAMA UNATUMIA IPHONE,UTAZITAZAMA GAME ZOTE MUBASHARA..
 
Back
Top Bottom