SportPesa Supercup updates.

Illa nimekuwa disappointed sana Na klabu za Tanzania. Wakati huu wote nilidhani Tanzania wametuzidi katika club football na wana klabu noma kutushinda kumbe uji baridi tu.

Maana imekuwa si TZ vs KE Tena. Ni KE Vs KE
 
sasa tumebaki kenya pekee Mashemeji derby ugenini Gor vs Ingwe(AFC Leopards)
 
Aisei Yanga yangu nje, haya bwana imebaki timu za Kenya. Duh! Hii inanikumbusha vile jinsi huwa kwenye riadha pale Kilimanjaro, kwamba namba moja moja hadi namba tano wote Wakenya, inakua kama tumeenda kushindana wenyewe kwa wenyewe kwenye nchi ya watu.
 
Kenya mmezishinda team B za simba na yanga msijitape sana
 
Mfano first eleven yote ya simba wachezaj wako na team zao za taifa. The same kwa yangu wachezaj 7 wote first 11 wako nje. Kingine team za bongo hazikujiandaa zilichukulia kama bonanza tuu ndo maana hata ma head coach tumewaruhusu waende kwa leave. Nyie wenzetu wa kenya kumbe mlikua mmepania sana. But all in all hongerani. Next time tuta take serious!
 
uninikumbusha utani fulani huwa hapa kenya ati ukicheza na timu kutoka coast mshinde utasikia ati aahh walitufunga lakini chenga walikula kweli.Sasa Tz wameanza vijisababu.
 
uninikumbusha utani fulani huwa hapa kenya ati ukicheza na timu kutoka coast mshinde utasikia ati aahh walitufunga lakini chenga walikula kweli.Sasa Tz wameanza vijisababu.
Umenena mkuu... Kama hawakuwa tayari wangesema
 
What sport is tanzania good at lakini???

Sasa Hapa mtasema Yanga ni Team B Pia??
 
Sio team tu mkuu..pia ni under 20. Cjui kwa nn hiv vilabu vimedharau haya mashindano. Kocha wa yanga anaulizwa kwa nn hajachezesha kikosi cha kwanza anadai anatafuta wa kuwapandisha first 11 na kujaribu wengine wapya. Ujinga tuu
 
Fifa ranking is just a number..ila mkija kwa pitch tunawanyuka tuu. Hio rank wala isikunyanyue mabega sio issue. Tuliipiga ghana na comeroon wenye rank za juu ni ninyi apo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…