Sports Extra Clouds FM tumieni muda vizuri

vevenononombo

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2015
Posts
1,289
Reaction score
421
Nimekuwa nikijiuliza kwanini watangazaji wa kipindi cha michezo Clouds FM sio weledi katika kutunza muda. Kipindi cha michezo ni kuanzia saa 3 hadi saa 3:59, lakini wamekuwa sio weledi kwani wanaweza kutumia hadi dakika 15 baada ya muda wao kuisha.

Jambo hili ni picha mbaya kwa taaluma ya habari na michezo pia kwani inaonyesha jinsi gani watu wasivyo makini katika muda. Badilikeni. Na huyo msimamizi wa vipindi ni mweledi kweli?

Mimi napenda kujipumzisha na miziki taratibu huku nikitafakari siku ilivyoenda. Jaribuni kubalika.
 
Blabla nyingi,nafikiri zimejaa,tz watangazaji licha ya kutumia muda vibaya wanatumia muda mwingi kwa mambo ya hovyo tu,utafikiri wapo mtaani
 
Nimekuwa nikijiuliza kwanini watangazaji wa kipindi cha michezo Clouds FM sio weledi katika kutunza muda. Kipindi cha michezo ni kuanzia saa 3 hadi saa 3:59, lakini wamekuwa sio weledi kwani wanaweza kutumia hadi dakika 15 baada ya muda wao kuisha.

Jambo hili ni picha mbaya kwa taaluma ya habari na michezo pia kwani inaonyesha jinsi gani watu wasivyo makini katika muda. Badilikeni. Na huyo msimamizi wa vipindi ni mweledi kweli?

Mimi napenda kujipumzisha na miziki taratibu huku nikitafakari siku ilivyoenda. Jaribuni kubalika.
Ahahahaha mkuu mbona umezunguka sana?.... Ila poa kwa sie werevu tumekuelewa ukipendacho.
 
Kumbe hata ww umeliona hilo..sio sports extra tu,hata vipindi vingine vingi huchelewa kuanza kikiwemo kipindi cha jahazi...big up to efm wao wapo punctual...
 
Mkuu sport extra ya sasa hv imepoteza ubora wake kabisaaaaa....!!!
 
Back
Top Bottom