Nimekuwa nikijiuliza kwanini watangazaji wa kipindi cha michezo Clouds FM sio weledi katika kutunza muda. Kipindi cha michezo ni kuanzia saa 3 hadi saa 3:59, lakini wamekuwa sio weledi kwani wanaweza kutumia hadi dakika 15 baada ya muda wao kuisha.
Jambo hili ni picha mbaya kwa taaluma ya habari na michezo pia kwani inaonyesha jinsi gani watu wasivyo makini katika muda. Badilikeni. Na huyo msimamizi wa vipindi ni mweledi kweli?
Mimi napenda kujipumzisha na miziki taratibu huku nikitafakari siku ilivyoenda. Jaribuni kubalika.