Katiba Mpya. Tukiwaambia kwamba katiba ni muhimu zaidi ya jambo lolote lingine. Ikifika kwenye masuala yanayohusiana na uongozi na maendeleo. Kwamba ni kichocheo nyeti cha kutimiza maono na kutekeleza ruwaza ya nchi, ya maika na mikaka ijayo. Huwa mnaishia kutuambia kwamba sijui sisi manyang'au tunapenda misifa.
Hiyo SRC ni taasisi huru ya kiserikali, ambayo ilibuniwa na katiba mpya ya Kenya 2010. Majukumu yake sio kupunguza tu mishahara ya wakubwa. Bali ni pamoja pia na kusawazisha mishahara na mapochopocho ya wadogo zao, kwenye ngazi tofauti, kulingana na kazi wanazozifanya. Zaidi ya yote huwa wanatoa mapendekezo ya kupandishwa pia, kwa mishahara ya wafanyakazi kwenye sekta tofauti nchini Kenya.
Viongozi wa taasisi hiyo sio vibaraka wa rais, kwasababu huwa hawachaguliwi moja kwa moja na rais. Ndio maana wana kiburi cha kutekeleza majukumu yao, bila uoga, kisa wanajua kwamba wanalindwa sawasawa na katiba. Hii kwa kimombo ndio huwa wanaita 'checks and balances'. Jambo ambalo ni muhimu sana na huwa linapunguza kwa kiasi kikubwa, kiburi na ulevi wa madaraka wa hawa viongozi. Ambao huwa tunawachagua wenyewe, sisi kina Wanjiku.