Ssebo ajiunga E FM

ridculouz

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
910
Reaction score
499
Mtangazaji maarufu nchini wa vipindi vya Radio na Television Dennis Busulwa a.k.a Ssebo amejiunga na Radio ya E FM ambayo imekwishajizolea umaarufu mkubwa jijini Dsm kwa kipindi kifupi tu kutokana na staili yake tofauti ya urushaji matangazo nchini.Ssebo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano kwenye vituo mbalimbali vya Radio na TV amejizolea sifa na mashabiki lukuki katika tasnia hii ya utangazaji kutokana na staili na vituko vyake awapo hewani.

"Mashabiki wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu nikiwa na E FM",alisema Ssebo.Ssebo anakutana na timu ya watangazaji wengine wakongwe kama Dj Majey, Dizzo One na Sos B waliokwisha anza kusikika Radioni hapo.

Source: http://www.jestina-george.com/2014/06/ssebo-ajiunga-e-fm.html?m=0
 
Huyo kwa sasa sio Ssebo bali ni Ndugu,keshakuwa Mtz
 
Unaweza kuta radio yake ndio kaiongezea mita band jana.
 
Hii radio efm ni nzuri ila wajipange kwenye watangazaji,bado hawashawishi.
 
Kwani ni mtanzania huyu jamaa?isije kuwa anacheza working permit na ukute asha oa ndugu yetu
 

Dah, sos b... Long time
 
Ndo leo naisikia hii redio..
mkuu hii redio ni mpya haina hata miezi 3 na huko kwenu mikoani bado haijaanza kusikika ila kwa dar kila mtu anijua wameipigia promo la kufa mtu, ukija Dar utasikia sifa zake
 
mkuu hii redio ni mpya haina hata miezi 3 na huko kwenu mikoani bado haijaanza kusikika ila kwa dar kila mtu anijua wameipigia promo la kufa mtu, ukija Dar utasikia sifa zake

Ina sifa gani zaidi ya kupiga miziki mwanzo mwisho? Ushabiki mwingne taaaabu kwelikweli...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…