dume kubwaaaa
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 255
- 28
Utaratibu wa kuwalazimisha wanachuo kutoka katika chuo hiki na matawi yake kulipa fedha za graduation hata kama mtu hataki kushiriki limetia doa chuo hiki na kuonekana kuwa ni biashara ya kulazimishana.Baada ya kuona kuwa watu wengi wanashindwa kuthibitisha kushiriki mahafari chuo hiki kilibadili mada na kudai ili upate transcript yako lazima ulipe shs 70,000/= hata kama hutashiriki graduation.Mimi nauliza mkataba wa chuo na mwanachuo ni mwanachuo kupata elimu na mwisho wa siku atunukiwe cheti chake baada ya kuhitimu na kufaulu,sasa suala la kuongeza gharama za transcript kutoka shs 10,000/= za awali hadi shs 70,000/= linakujaje?
Jamani wenye mamlaka na masuala haya mtusaidie ili sisi watanzania maskini tusiendelee kunyanyaswa
Jamani wenye mamlaka na masuala haya mtusaidie ili sisi watanzania maskini tusiendelee kunyanyaswa