nENDA KAMWELE MKUU WA SHULE ,USIANDIKE HAPA UNLESS UNATAKA KUMWARIBIA BIASHARA.NENDA STRAIGHT SHULENI KWAO PELEKA MALALAMIKO
Pole basi kama shule yenyewe haisikilizi malalamiko ya wazazi inabidi uchukue hatua ,ama kumwamisha mtoto au kuripoti polisi pindi uonapo gari limejaa na watoto wamesimama.Watoto ni kama abiria wengine tu sheria inasema wote wanatakiwa wawe kwenye vitu .Sasa hapo kwa jeshi letu huwa wawazingatii hii sheria kabisa watakuambia kuna upungufu wa mabasi au rasilimaliNipeleke malalamiko mara ngapi ndio nije kuandika hapa. Malalamiko kwa maandishi na mdomo wala si mara moja. Hapa ni just ku share na wazazi wenzangu na wewe si lazima uchangie
Kwanza, mabasi ya wanafunzi ya shule hii ni mabovu kiasi cha kushangaza kiasi cha kutishia usalama wa watoto wetu.
Pili, Wanafunzi wanajaa sana kwenye mabasi kinyume na sheria za usalama barabarani ilhali wote wamelipa hela sawa ya usafiri. Pata picha mtoto mdogo wa darasa la kwanza au pili aliyeamka saa 11 alfajiri akiwa anarudi nyumbani saa kumi jioni amechoka huku amesimama na gari ikitumbukia katika barabara mbovu za sinza zenye mahandaki. This is not fair!
Je? huu ni uungwana?
Niseme ni mpangilio mbaya tu wa route na gari kuwajibika kuwapitia watoto weeengi. Nilimpeleka mtoto shule hiyo nikijua sinza na mikocheni ni karibu hivyo hataamka mapema matokeo anachukuliwa saa 12 kamili na anazunguka kwenye gari mpaka 1.30 ndio anafika shule. Na mashimo ya sinza basi ni balaa. Naamini kama gari ingebeba wanafunzi wachache maana yake angechukuliwa hata moja kasoro ila ndio shule iko kibiashara zaidi na si haki.
gari ikibeba wanafunzi wachache means you have to pay more to cover the fixed running costs.
Halfu issue nyingine wazazi pia muwajibike, kwani ni lazima utumie school bus kupeleka mwanao shule? Je umeshawasiliana na wazazi wenzio wenye watoto shuleni hapo mkajadiliana cha kufanya kuepukana na matatzio hayo ya usafiri? Au mnaendelea kuvumilia hadi janga litokee?