Staa wa The Shield amuua mke wake

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
1,633
Reaction score
560
Aliyekuwa staa ya series maarufu ya The Shield, Michael Jace ametiwa mbaroni kwa kosa la kumuua mke wake. Staa huyo alijisalimisha polisi baada ya kumuua kwa kumpiga risasi aliyekua mke wake,April Jace, imerepotiwa.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 48 alikiri kumpiga mke wake risasi mara kadhaa baada ya ugomvi mkubwa uliotokea pale mke wake April, aliporudi nyumbani.

April alikua anarudi na watoto baada ya kuwachukua kutoka kwenye mazoezi ya kikapo.

Imesemekana kua muigizaji huyo alikua na hasira juu ya matumizi ya pesa aliokua akifanya mke wake licha ya hali yao ya kifedha kuwa mbaya.

Imeripotiwa kua hali yao ya kifedha ilikua mbaya mpaka kufikia kushindwa kulipia ada ya pango ya mwezi, sababu ambayo polisi wanahisi ilimfanya muigizaji huyo kupandwa na hasira na kuamua kumtolea mkewe.

Muigizaji huyo anajulikana zaidi kwa kuigiza kwenye series ya The Shield, Southland, Burn Notice pamoja na The Mentalist.

Muigizaji huyo ambae alizaliwa New Jersey nchini Marekani pia amewahi kuonekana kwenye filamu za Forrest Gump na Planet of the Apes ya mwaka 2001.

 

Attachments

  • michael-jace-and-wife.jpg
    10.8 KB · Views: 986
Inawezekana jamaa ana asili ya mkoa fulani wa kaskazini.
 
Huko hua hawataki upumbavuuu chezeaaa
 
Inawezekana jamaa ana asili ya mkoa fulani wa kaskazini.

Si bure una lako jambo umekataliwa nini na mshua wa kule sie kikawaida hatupendi wanaume mazuzu kama vipi tupa kule
 
mambo ya ufoooo sarooooooooooo mpaka majuu, kina mushi wapo wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…