Stability ya Serikali inategemea mgombea urais achelewe kuteuliwa

Stability ya Serikali inategemea mgombea urais achelewe kuteuliwa

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Rais Samia angechaguliwa May kuwa mgombea urais ingeleta maana zaidi.
Sasa hivi serikali inakosa legitimacy. Serikali inakosa uhalali.
Hakuna ushindani,hakuna struggle,njia za mkayo zinatumika kuingia Ikulu au kukaa Ikulu.

Rais anaingia uwanjani na mtu anatembea MBELE ya gari. Whatever does that mean? This is shocking. Official endorsement ifanyike katika Mkutano wa baadaye wa Chama na hii arrangement ya sasa ihesabike kwamba ni kitu tentative.

Again people should be reminded. Watu hawakumchagua huyu Rais. Watu walimchagua Magufuli. Na huyu Rais hawezi kuingia Ikulu kwa njia za mkato. Lazima aingie Ikulu the old fashioned way. Hivi ndio Kamala Harris slivyoshindwa Uchaguzi.

Inaweza vipi kwenda kwa bride amesimama kwenye altare kwamba," Bwana arusi amepatwa na udhuru. Nimekuja mimi badala yake" Hata Unguja yule mtu mmoja aliingia matatani kwa kusema Hussein Mwinyi hakufika Unguja hata siku moja kufanya Kampeni,walisikia tu ametangaza na Kamati Kuu kuwa atakuwa mgombea urais Zanzibar.

Imetosha huyu Samia kuwa Rais. Siku alizokuwa Rais zinatosha.
 
Rais anaingia uwanjani na mtu anatembea MBELE ya gari. Whatever does that mean? This is shocking.
Official endorsement ifanyike katika Mkutano wa baadaye wa Chama na hii arrangement ya sasa ihesabike kwamba ni kitu tentative.
Again people should be reminded. Watu hawakumchagua huyu Rais. Watu walimchagua Magufuli.
Na huyu Rais hawezi kuingia Ikulu kwa njia za mkato. Lazima aingie Ikulu the old fashioned way.
Hivi ndio Kamala Harris slivyoshindws Uchaguzi.
Inaweza vipi kwenda kwa bride amesimama kwenye altare kwamba," Bwana arusi amepatwa na udhuru. Nimekuja mimi badala yake"
Hata Unguja yule mtu mmoja aliingia matatani kwa kusema Hussein Mwinyi hakufika Unguja hata siku moja kufa Kampeni,walisikia tu ametangaza na Kamati Kuu kuwa atakuwa mgombea urais Zanzibar.
Imetosha huyu Samia kuwa Rais. Siku alizokuwa Rais zinatosha.
Naona ile changamoto yako inaelekea ukingoni Mkuu, unamwaga nondo sana siku hizi.
 
Trump husema hizi ni DEI hire, alikua DEI hire from the beginning sasa unataka DEI ishindanishwe na merit halafu atoboe kweli?
 
Rais Samia angechaguliwa May kuwa mgombea urais ingeleta maana zaidi.
Sasa hivi serikali inakosa legitimacy. Serikali inakosa uhalali.
Hakuna ushindani,hakuna struggle,njia za mkayo zinatumika kuingia Ikulu au kukaa Ikulu.

Rais anaingia uwanjani na mtu anatembea MBELE ya gari. Whatever does that mean? This is shocking. Official endorsement ifanyike katika Mkutano wa baadaye wa Chama na hii arrangement ya sasa ihesabike kwamba ni kitu tentative.

Again people should be reminded. Watu hawakumchagua huyu Rais. Watu walimchagua Magufuli. Na huyu Rais hawezi kuingia Ikulu kwa njia za mkato. Lazima aingie Ikulu the old fashioned way. Hivi ndio Kamala Harris slivyoshindwa Uchaguzi.

Inaweza vipi kwenda kwa bride amesimama kwenye altare kwamba," Bwana arusi amepatwa na udhuru. Nimekuja mimi badala yake" Hata Unguja yule mtu mmoja aliingia matatani kwa kusema Hussein Mwinyi hakufika Unguja hata siku moja kufanya Kampeni,walisikia tu ametangaza na Kamati Kuu kuwa atakuwa mgombea urais Zanzibar.

Imetosha huyu Samia kuwa Rais. Siku alizokuwa Rais zinatosha.

Watanganyika ni lazima tuonyeshe kuwa hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanganyika hii iliyopigiwa uhuru na Mabau zetu .
Wazanzibari wana nchi Mbili wengine tatu pamoja na Oman.

Tanganyika kwa Wazanzibari ni nchi yao .
Lakini pia baadhi ya wazanzibar Oman pia ni nchi yao .
Lakini Watanganyika kutoka kule Dodoma mpwapwa ,Shinyanga ,Mpanda ,Ngorongoro, Iringa n.k Hawana nchi nyingine ya kukimbilia zaidi ya Tanganyika .
Kuendelea kuruhusu familia mbili kuichezea ni ujinga mkubwa na kuvikosea vizazi vyetu haki .

Tuna Rais ambaye hata uhalali wa kuwapatanisha wakongo na M23 hana maana alitaka kutuletea hatari kama inayotokea Kongo kwa kuuza ardhi yote ya Wamasai na kujaribu kuwafukuza huku akiweka wapambe kama akina Shekhe Mwaipopo kusema kuwa wale wamasai wanaopinga kuondoka Ngorongoro sio Watanzania, ni Wakenya . Bahati nzuri TLS ,Tundu Lisu na Askofu Mwamakula wakasimama Kidete kupinga hilo jambo ambalo kama sio kuwa na Jeshi imara huenda lingetuletea vita ya wenyewe kwa wenyewe . Maana hata huko ndani ya Majeshi kuna Wamasai japo ni wachache ambao wasingefurahi kuona ndugu zao wakiuawa na kupigwa kwa sababu ya waarabu na wazungu wanaopora ardhi ya umma kwa kushirikiana na watawala tena kutoka visiwani wasiojua shida ya ardhi kwa Wafugaji kama ilivyo shida za kibiashara kwao .

Nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanganyika inahitaji Rais asiye mbinafsi na mpenda mali kupitiliza na anayeiweka familia yake mbele badala ya mamilioni ya watu . Anatakiwa Rais ambaye hatuwezi hata kujua kuwa ana ndugu au watoto au marafiki ! Tunahitaji Rais ambaye kwake Tanzania kwanza na Kikatiba ya nchi ndiyo mwongozo na sio hisia na itikadi zake .

Tunahitaji Rais ambaye Fursa za kiuchumi ziwe zinatolewa kwa wote sio kwa misingi ya vyama au dini .
Kama mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba ni mizuri na inampa mtu unafuu wa maisha na kukuza mtaji basi Watanganyika wote wapewe badala ya kuweka itikadi za kichama na kidini kwenye uchumi . Huu ni ubaguzi wa wazi kwa Watanganyika na watanzania kwa ujumla . Rais awe ni Mzalendo namba moja kuhakikisha keki ya Taifa inawafikia wanyonge na pawe na mfumo wa kuhakikisha hilo linafanyika na anayepinga na hilo anatolewa haraka . Leo Mfano Kafulila ni mpiga debe tu hana mkakati wowote wa kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na Gesi ,madini ,ardhi,wanyama ,utalii,makazi ,misitu na samaki na hata maji na bei ndogo ya nishati au mawasiliano lakini hatuoni mpango huo zaidi ya kushinda kwenye mtandao wa X na kusifia sifia tu jambo ambalo halitusadii zaidi ya kuweka mbele maslahi yake na ya bosi wake tu kisiasa .

Kama tuna Rais anayewaza kushinda tu uchaguzi wakati hakuwahi kugombea basi tujue wazi kuwa Kuna maslahi yake anayopambana kufa na kupona kuyalinda .

Rais Mzalendo ni yule anayefanya jambo hata kama atakosa kura lakini asimamie haki na kupinga rushwa .

Kama tuna Rais anayotoa rushwa ili ashinde uchaguzi na jamii imeshazoea hivyo tutawezaje kuzuia wizi wa mali za umma .
Bora Mugabe alikua anashinda kwa nguvu ikazoeleka kuliko ushindi wa Rushwa . Rushwa inaleta watawala wala rushwa na wanaoiba na kufuja mali za umma .

Huyu Mtu alikua kama tingo wa basi lenye Dereva . Tingo Ambaye kimsingi hakuwa amechaguliwa na dereva wala abiria wala mwenye basi, zaidi ya wapiga debe(Kimsingi ni Tingo aliyechaguliwa na wapiga debe) .
Kwa bahati mbaya Dereva akafariki njiani ,Ikabidi Tingo aendeshe gari kwa sababu alikua na leseni ya udereva.
Ndugu na marafiki na wapiga debe waliokua wamempiga debe awe tingo wakaona ni fursa kwa ndugu na rafiki yao kupata kazi ya udereva kirahisi kabisa.
Cha ajabu hawataki nafasi ya ajira ya udereva itangazwe wala ifanyiwe interview, hata ndugu wa Tajiri hawataki wapewe nafsi ya kutafuta dereva wanayemwamini na kuona ana uwezo zaidi.
Abiria wengi wakatoa maoni yao kuwa uendeshaji wa Tingo sio mzuri maana wakati mwingine hata alama za barabarani hazijui mpaka aulize abiria .
Kutokana na maslahi ya ndugu na marafiki basi Tingo anapambaniwa ili awe dereva na asiajiriwe dereva mwingine .

Mbaya zaidi pesa alizokuwa amekusanya zote anazitumia kuwapa wapiga debe ili wapigie debe kwa tajiri na kusema kuwa ndiye anayefaa kuwa dereva . Pesa za tajiri akazitumia zote kupambania nafasi ya udereva na alipouliza na tajiri pesa ziko wapi akamsingizia kuwa alikua amemkabidhi dereva aliyekufa .

Baada ya kufika mwisho wa safari kwa mashaka mashaka na kwa bahati bahati Sasa gari linataka kuanza safari tena. Abiria wengi hawana imani na udereva wa Tingo wanamuomba mmiliki wa gari aajiri dereva mwenye uwezo zaidi . Lakini wapiga debe stend na marafiki wa Tingo kwa sababu ya asali anayowalambisha anafanya fujo ili Tingo ndiye apewe gari kwa sababu tu ni rafiki yao na wamemzoea .Wao hawajali maisha ya abiria zaidi ya maslahi yao na Tingo wao .

Sasa abiria wengi wanataka kushuka na kupanda basi lingine kwa ajili ya usalama wao .
Sasa ni ama tajiri amtoe Tingo na kuleta dereva mwingine au akubaliane na wapiga debe halafu apate hasara ama gari ipate ajali kabisa kutokana na uendeshaji mbovu wa Tingo .
Ningekua mimi ningemshauri Tingo asiwasikilize wapiga debe wala asiangalie maslahi yake bali aangalie matakwa ya wateja ambao ni abiria wanaompatia nauli .
Kwa Tingo huyu Abiria watafika lakini wakiwa wamechoka sana.
 
Back
Top Bottom