Wapo wana hip hop wengi wa zamani waliofanya vizuri lakini leo hii game yetu imeshikiliwa hasa na hao vijana wanne tajwa hapo juu.Napenda sana kusikia nyimbo zao redioni ila sema ndio hivyo tena wabana'mhhhh' wamekaba sana kiasi kwamba ni nadra kuwasikia redioni lakini sisi wadau tunajua wapi tutazipata tu.Hebu nipe tafakuri yako mdau wa hip hop ni yupi kati ya Stamina,One,Stereo, na Songa unafikiri ni mkali zaidi kwa kuandika na kuimba ikiwezekana weka punch line moja kutoka kwenye nyimbo zao kusuport point yako.