Stand ya mkoa ubungo kuwa na mlango mmoja wa kutoka ni sawa?

Stand ya mkoa ubungo kuwa na mlango mmoja wa kutoka ni sawa?

BENNO URASSA

New Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
4
Reaction score
0
Jamani watanzania hivi hii stand yetu ni sawa kuwa na mlango mmoja tu wa kutoka magari au mpaka litokee balaa humu ndio tuanze kutafuta wa kumlaumu hata ukija alfajiri hapa wakati wa kutoka mabasi na abiria ni fujo tupu sasa je ikitokea tatizo humu ndani si maafa ya kutisha yatatokea hapa stand watu na mali zao?.mimi nashauri iongezwe milango ya kuingia na kutoka na iwe kwa kanda mfano tanga arusha moshi mlango wao nakadhalika.
 
Ile stand ilishapitwa na wakati, inafaa kuwa gereji tu. Stand gani imechoka mbaya, ile kodi ya ushuru inayokusanywa inafanya kazi? Kwa nini wasihamishie sehemu nyingine ya nzuri kubwa na yenye kutoa huduma vizuri? Hapo haifai hiyo stand, mfano angalia hao makampuni makubwa hawapaki ndani ya hiyo stand siku hizi.
Ubungo stand inafaa ijengwe shopping complex kubwa siyo stand inayotunza wazembe wa kufanya kazi aka wezi, vibaka.
 
Jamani watanzania hivi hii stand yetu ni sawa kuwa na mlango mmoja tu wa kutoka magari au mpaka litokee balaa humu ndio tuanze kutafuta wa kumlaumu hata ukija alfajiri hapa wakati wa kutoka mabasi na abiria ni fujo tupu sasa je ikitokea tatizo humu ndani si maafa ya kutisha yatatokea hapa stand watu na mali zao?.mimi nashauri iongezwe milango ya kuingia na kutoka na iwe kwa kanda mfano tanga arusha moshi mlango wao nakadhalika.
Lakini umefikiri vyema kwa hilo unalolilalamikia?.
Kila mkoa mlango wake labda na wa kuingilia pia.Nani atalipa walinzi wa mageti yote hayo,au itabidi ada za magari ziongezwe na abiria wachangie.
Hilo tatizo unalolihofia sioni kwamba ni zito katika eneo la wazi kama lile.Kwanza hakuna msongamano wa hii..vyo.Halafu mambo yakizidi ni rahisi kuchupa na kutoka kwenye zile kuta ukiweka kitu kidogo tu cha kusimamia.
 
Back
Top Bottom