Stanslaus boniface afariki dunia

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
NI YULE MWENDESHA MASHTAKA KESI ZA EPA, R I P BROTHER.
MKURUGENZI Msaidizi wa Mashitaka nchini na Mwendesha Mashitaka mashuhuri katika kesi kubwa mbalimbali nchini, Stanslaus Boniface amefariki ghafla.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana mchana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, Boniface alifariki ghafla jana asubuhi na chanzo cha kifo chake hakijafahamika.

"Boniface amefariki leo (jana) alfajiri katika Hospitali ya Regency alikopelekwa baada ya kujisikia vibaya akiwa nyumbani kwake…msiba upo nyumbani kwake eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," alisema Ofisa Habari wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (AG), Siatu Msuya.

Boniface alipata umaarufu katika kesi alizokuwa akiziendesha ambazo ni za wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT) ikiwamo inayomkabili kada wa CCM, Rajab Shaban Maranda na wafanyakazi wanne wa BoT wanaodaiwa kuiba Sh

Nyingine ni ile ya wizi wa Sh bilioni 1.1 inayomkabili Bahati Mahenge na wenzake wanne.

Boniface alizaliwa Februari 21, 1968 na ameacha mke na watoto watatu. Amewahi kufanya kazi kama Mwendesha Mashitaka Mkuu katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam,

Waungwana nani anajua mahali ulipo msiba? Nyumbani kwake Chuo kikuu haitoshi. ni bora tukapata maelekezo zaidi. RIP ndugu yangu Stan
 
Waungwana nani anajua mahali ulipo msiba? Nyumbani kwake Chuo kikuu haitoshi. ni bora tukapata maelekezo zaidi. RIP ndugu yangu Stan

MSIBA UPO

UDSM kwenye nyumba za lecturers, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mtaa wa Sinza Load Kitalu Na. 4 ni nyumba ipo jirani na UDASA CLUB ilipo...ukifika tu pale UDASA karibu na mlimani primary school utaona watu wengi
 
MAZISHI ni kesho JUMANNE, MSIBA UPO

Poleni sana kiongozi. Tupo pamodja.

Mungu amrehemu Mpiganaji Stan. Tumepoteza mtu muhimu sana kwenye tasnia ya Sheria nchini, mtu aliyejitoa moyo wake wote kutumikia taifa hili, aliyekubali kufia nchi yake kwa kutumia akili yake. Mara zote alikuwa mfano wa wale waliomfuata.

Matendo mema yana dhihirisha....wengi wanajua alivyokuwa mpiganaji.

R.I.P

Kaka umetangulia, tuko nyuma yako. Ulikuwa kioo chetu katika kusaka elimu.Isanga na Iganzo(Kwa macho) Mbeya ambako kuna mji wako wanakukumbuka.Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi. Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…