Staphylococcus aureus

Staphylococcus aureus

samakinchanga

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
2,024
Reaction score
1,233
Jamani waganga na waganguzi nisaidieni huo hapo ugonjwa nimeambiwa umekuwa immune kwa antibiotics kama amoxcline,ethromicyne,cipro,chrolophenicol na nitrotarantoin na mwili sasa una rashes nitumie dawa gani?na nini chanzo chake?

Mzizi mkavu na wengineo msaada hapo haraka
 
S. aureus sio ugonjwa ila ni aina ya bacteria ambao wapo kwenye ngozi za binaadamu wote.
Wadudu hao wanaweza kushambulia kidonda au kuingia kwenye njia ya mkojo na kuleta matatizo.
Wapo S. aureus wa aina nyingi, kwa hiyo matibabu yake iwapo wameingia kwenye kidonda au njia ya mkojo inategemea na aina uliyokuwa nayo.

Nini cha kufanya: Inahitajika kufanya kipimo cha microbiology cha kujua aina ya bakteria uliokuwa nao na dawa inayoweza kuwatibu ( culture and sensitivity).

Vileviel, wadudu wowote huweza kumshambulia zaidi mtu mwenye upungufu wa kinga. Hivyo basi, iwapo unapata matatizo ya infections mara kwa mara ni vyema ukafanya vipimo zaidi ili kuona kama kinga ya mwili wako iko sawa.
 
Hiyo itakuwa ni Methicilin Resistant Staphylococcus Aureus (MRSA)
Kwahiyo tumia antibiotics zisokuwa na beta lactam ring!!!
 
Aves nipe walau sample za hizo dawa maana mmh siko vizuri.
 
Nenda kaonane na daktari wa ngozi kabisa kama hizo rashes ndio tatizo.

Sijui wamepima vipi kukupa maelezo hayo.

Hata kama ni culture bado dawa hizo kwa wadudu hao zina walakini.

Fanya uonane na daktari wa ngozi. Si ajabu wanatibu maambukizi lakini tatizo lako likawa siyo hilo.
 
Hiyo itakuwa ni Methicilin Resistant Staphylococcus Aureus (MRSA)
Kwahiyo tumia antibiotics zisokuwa na beta lactam ring!!!

Angalia vizuri hiyo list ya dawa, Beta lactam ziko ngapi.

Halafu rudi kwenye criteria za MRSA . Hapo hata Methicilin haipo.
 
kama mdau alivyosema hapo juu hio itakua ni methicillin resistant staph, sasa dawa ambayo inaonekana kutibu hii kitu ni vancomycin, nadhani hii dawa bado haija develop resistance kwa huyu mdudu...
 
Hii misamiati hapa haipo kichwani mwangu kabisa. But i am learning something
 
dawa kama ampiclox. ampicillin+cloxacillin hutibu hii ishu ila wengi hupata reinfection hasa kutoka kwenye mataulo

mkuu hizi dawa kwene huyu mdudu zinadunda hata vancomycin haina madhara dawa kali karibu zote
 
Ulifanikiwa kupata tiba yake ??
Msaada fadhali ananisumbua huyu mdudu
 
Back
Top Bottom