S. aureus sio ugonjwa ila ni aina ya bacteria ambao wapo kwenye ngozi za binaadamu wote.
Wadudu hao wanaweza kushambulia kidonda au kuingia kwenye njia ya mkojo na kuleta matatizo.
Wapo S. aureus wa aina nyingi, kwa hiyo matibabu yake iwapo wameingia kwenye kidonda au njia ya mkojo inategemea na aina uliyokuwa nayo.
Nini cha kufanya: Inahitajika kufanya kipimo cha microbiology cha kujua aina ya bakteria uliokuwa nao na dawa inayoweza kuwatibu ( culture and sensitivity).
Vileviel, wadudu wowote huweza kumshambulia zaidi mtu mwenye upungufu wa kinga. Hivyo basi, iwapo unapata matatizo ya infections mara kwa mara ni vyema ukafanya vipimo zaidi ili kuona kama kinga ya mwili wako iko sawa.