Star link yapigwa zengwe, makampuni ya simu hayaitaki

Lakini stratlink ni satelite internet..na ukifunga inakuwa ni stationery, yaani siyo mobile. Bei yake pia iko juu kidogo kuliko stationery internet zinginene unazoweza kupata maeneo ya mijini.

Je ni kwa namna gani inaweza kuharibu soko la mobile internet kama za Voda, airtel, tigo n.k.

Mimi naona watu wana mihemuko kwenye hili swala bila kujua what is offerred by starlink..Watu wanadhani unaweza kupata internet kwenye simu ukiwa unatembea. May be hili linaweza kuja lakini siyo hivi karibuni.

Starlink itafaidisha mazingira ambayo internet connection zingine hazipatikani..kama maeneo ya vijijini
 
Umewahi kuitumia kwa hapa tz? Tytajie hiyo bei
 
Umewahi kuitumia kwa hapa tz? Tytajie hiyo bei
Kule USA bei ya starlink ni $115 gharama ya vifaa na installation ni $500

Kwa Nigeria bei ya starlink ni $43(ambayo inakaribia laki) na bei ya vifaa ni hiyo hiyo yaani shilingi 1,159,049.50


Hapa Tanzania kuna zuku ambayo ni shilingi 79,000 Kwa mwezi, ttcl faiba 55,000, kuna konect 60,000 Ila installation bei inafika milioni, Vodacom supakasi 115,000, na bado idadi ya wateja ni ndogo.

Sasa sijui hiyo starlink inakuja kupunguzaje gharama za intaneti na sioni kuwa ni tishio Kwa mitandao nchini kutokana na gharama kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…