Ninachokijua kuhusu huyu jamaa, alibahatika kupata zengwe la TBL karibia mitano sasa imepita alivyokuwa Arusha aliripoti taarifa ya hawa TBL (huhusu chupa ya bia) ilikuwa na mende na uchafu mwingine na chupa ilikuwa haijafunguliwa waliokuwa wanatumia hicho kinywaji wakamuita jamaa akapiga picha na kutuma kwa Mhariri wake bila kutoka kwa wiki moja.
Mwoleka akampigia bosi wake akiulizia mbona hiyo story haikutumika? hii ilitokana na kwamba mara nyingi watumiaji wa kinywaji hicho walikuwa walilalamikia hali hiyo kwa muda mrefu. Itakumbukwa kipindi hicho TBL walikuwa wanadhamini sana vipindi vya Sahara Media wamiliki wa (Star TV, RFA, na Kiss Fm) akaelezwa kuwa kutokana na hali ilivyoilikuwa ngumu kuwalipua watu wanaozamini vipindi na hapa ieleweke kuwa Media yeyote inaendeshwa kwa matangazo.
Kilichofuatia jamaa alikomaa kwamba story itoke kwamaana wamevurunda wenyewe, simu ikapigwa Dar es Salaam (makao makuu ya TBL kwa wakati huo sijui sasa) kueleza hali ilivyokuwa ikaulazimu uongozi kuruka Mwanza mara moja na Mwoleka kukatiwa tiketi ya Ndege mara moja (inaelezwa kuwa ndio mara yake ya kwanza kupakia Ndege) ndipo zikatolewa bahasha mbili mlungula wa milioni 2, ila Mwoleka akaikataa na baadae kuikubali kwa shingo upande kuanzia hapo mambo yakaanza kumwendea mrama....akafungua gazeti la Kutoka Arusha lilikuwa la Mkoa wa Arusha tu sijui hadi leo lipo au limekufa.................