Star wa 12 years a slave Chiewetel Ejiofor kuwa kubwa la maadui kwenye movie ya James Bond

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Nyota wa filamu ya 12 Years A Slave, Chiewetel Ejiofor huenda akapata mchongo mkubwa zaidi kwa kushiriki katika filamu maarufu duniani ya James Bond.

Watu wa karibu na watayarishaji wa filamu mpya ya James Bond iliyopewa jina la ‘Bond 24’, wameuambia mtandao wa TheWrap kuwa hivi sasa watayarishaji hao wameelekeza macho yao kwa Chiwetel Ejiofor kuchukua nafasi ya mhusika anaepambana/anaempinga mhusika mkuu Daniel Craig. Kwa lugha ya uswahilini tunamuita ‘kubwa la maadui’.

Vyanzo hivyo vimeeleza kuwa mbali na kumtafuta muigizaji wa kiume, waandaaji wa Bond 24 pia wanamtafuta muigizaji wa kike mpya atakayekuwa na kazi kubwa katika filamu hiyo.

Hata hivyo, imesemekana kuwa tayari waigizaji waigizaji wawili wa kike wa Sweden Ida Engvoll na Disa Ostrand wamefanyiwa majaribio kwa ajili ya kushiriki katika filamu hiyo.

Bond 24 itakayoongozwa na Sam Mendes inatarajiwa kuanza kushutiwa August mwaka huu, na imepangwa kutoka November 6, 2015.
 
Kuna kitu najiulizaga kuhusu muvie industry hasa hollywood sijapata majibu, siku nikiwa na muda ntakileta tukijadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…