STAR WARS yamnyakua Lupita Nyong'o

STAR WARS yamnyakua Lupita Nyong'o

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
140303065035_lupita_512x288_reuters.jpg
Lupita Nyong'o kung'aa zaidi


Msanii muigizaji kutoka Kenya Lupita Nyong'o ameteuliwa kuijiunga na mabingwa wengine wa kimataifa katika filamu maarufu zaidi duniani STAR WARS.

Lupita anatarajiwa kuonekana katika kipindi cha saba msimu huu wa Star Wars. Hii inafatia ufanisi mkubwa aliopata katika filamu '12 years a slave', ambapo alinyakua taji la Oscars la muigizaji bora msaidizi.
140603003022_gwendoline_christie_512x288_bbc.jpg
Gwendoline Christie


Msanii mwingine aliyetajwa kujiunga na 'star Wars' ni Gwendoline Christie,ambaye kwa sasa anatambulika zaidi katika mchezo wa televisheni wa 'Game of Thrones' unao endelea kupata umarufu duniani. Yeye pia ataonekana katika filamu ya 'Hunger Games'.
"Nashindwa kuelezea furaha yangu kwa Lupita na Gwendoline kwa kujiunga na waigizaji wengine katika kipindi hiki cha Star Wars.,'' amesema Kathleen Kennedy, rais wa kampuni ya Lucasfilm inayosimamia utengezajiwa filamu hiyo.
[h=2]Wengine waliotajwa[/h]Waigizaji wengine wapya watakao jiunga katika kpindi hicho ni John Boyega, Daisy Ridley, Adam Driver, Oscar Isaac, Andy Serkis, Domhnall Gleeson, na Max von Sydow. Wale wa awali tangu mwanzo ni Harrison Ford, Carrie Fisher, Mark Hamill, Anthony Daniels, Peter Mayhew, na Kenny Baker.
Star Wars: Kipindi cha VII inasimamiwa na J.J. Abrams na kuelekezwa kuwa filamu baada ya kufanya vyema kama kipindi cha televisheni kwa muda mrefu.
Filamu hiyo inatarajiwa kuwa tayari kuoneshwa katika sinema kuanzia tarehe 18 Disemba, 2015.

STAR WARS yamnyakua Lupita Nyong'o - BBC Swahili - Habari
 
Back
Top Bottom