Starehe zamponza Okrah

KENGE 01

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
1,705
Reaction score
4,217
Mwamba wa ghana kipaji anacho kizuri tu. Sasa shida ni starehe zimezidi inadaiwa baada ya kutua jiji la starehe za aina zote DAR ES SALAAM, Okrah amekua ni mtu wa maji sana.

Tafiti za kimatibabu ndani ya Simba zimeonesha Okrah ndio mchezaji anaangoza kwa fatique(Kubanwa msuli uwanjani) ndani ya muda mfupi kuwahi kutokea. Fatigue zinasababishwa na mambo mbalimbali kwa Athletics ikiwemo mazoezi hafifu.

Injury pia zilimuandama kwahiyo trip moja uwanjani nyingine hospital. Vilevile Kupigana na wachezaji wenzie.

Okrah ameonekana mara kadhaa akishinda kidimbwi usiku kucha. Inadaiwa wakala wake ametuma Ofa kwa Yanga hivyo anasubiri wakae mezani.

Simba imetangaza kuboresha kikosi kwa kuachana na baadhi ya wachezaji wake akiwemo Mkude, Kyombo, Kapama n.k

Starehe zisizidi kiasi

Nawasilisha
 
Kwahiyo Boko ataendelea kubakia Simba, hakika Simba hatuna dhamira ya mabadiliko.

Unamuacha Okrah then unabakisha Boko.. huu ni upuuzi uliofanya tufe kiume kwneye mechi ya Wydad.. yani team inahitaji matokeo alaf anaingia boko badala ya moses phiri.

Kwa kasi waliyonayo utopolo, tunaweza kuutafuta ubingwa mpaka 2025 tusipokuwa makini. Mabadiliko ndani ya Club lazima yahusishe kutoa wachezaji wazee likes of Boko na Nyoni.. hao ndio wapiga misumari wakubwa
 
Legend haachwi kizembe soon atasaini mkataba wa Mitano tena
 
Sio, mfuatiliaji sana, wa maisha binafsi ya mchezaji lakini nitakuwa, wa, mwisho kuamini kuwa ulevi ndo sababu, ya kushuka kwa kiwango Chake na kupelekea kuvunjwa kwa mkataba wake.
Ndipo wahenga wakasema "Usilolijua ni sawa na......"
 
Hebu mtaje mchezaji kijana mwenye uwezo kumzidi Boco..Kyombo ndio huyo..Haya Nyoni nae amekuwa bora kuliko Kapama..acha tu waendelee kula pensheni vijana wameshindwa.
 
Yanga ya sasa siyo zoazoa, usifananishe Yanga hii na vitu vya kipuuzi.
 
Sidhani kama ni starehe ila simba inabidi ifanye tathimin ya watu wa physical haiwezekani kila mchezqji akipata majeruhi inakuwa ngumu kutudi kwenye form aliokuwa nayo.
Refer kwa moses phiri na okrah mwanzo wa msimu hofu yqngu hata aishi akirudi kutakuwa na tatizo
 
Tatizo la Okrah hapo Simba sio ulevi bali ni uchawi kwa wachezaji, kwahiyi Israel nae ni mlevi?, Vipi phili, Banda?. Kingine Okrah Karma yakutumika kumfukuza Dejan inamtafuna, Yanga Kama wanataka Winga basi Okrah anafaa.
 
Mchezaji hapangwi halafu wanasema ameshuka kiwango, kama ulevi ingekuwa sababu hukuwaona Kizota, Gaga na Mafisango tukubali Simba Kuna tatizo ndio maana Kuna msimu Boko alimaliza bila kufikisha goli tatu na pia ni majeruhi mara kwa mara lakini Kila msimu anaongezewa mkataba
 
Kwa wachezaji waliopo simba ilihuraji beki na kiungo mmoja tu. Kwasababu pale mbele pako vizur
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…