Starlink wakipewa kibali, hii mitandao ya simu itashika adabu

Starlink wakipewa kibali, hii mitandao ya simu itashika adabu

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
Yaani natumia router ya airtel, na Voda kwa lengo lakuwa na internet ofisini lakini kuna muda mitandao yote tabu lele,leo siku nzima inasuasua tu ,

Nimeamua kutafuta pocket router ya Tigo ndio angalau naweza ku access,wamenikwamisha pm zangu nyau wale,STAR LINK wapewe kibali muone utamu wa kupoteza wateja ili akili ziwakae sawa ,Filho da puta!

Soma Pia: Mitandao ya Simu yadaiwa kuilalamikia Starlink kwa kuongeza ushindani Sokoni
 
Tena waruhusiwe haraka, hii mitandao ina gharama za juu sana na wizi tele wa mabando.
 
Hicho kitu sidhani kama kitakuja tokea sababu Serikali yenyewe inashiriki kutunyonya wananchi wake kupitia hiyo mitandao uchwara.
 
Hicho kitu sidhani kama kitakuja tokea sababu Serikali yenyewe inashiriki kutunyonya wananchi wake kupitia hiyo mitandao uchwara.
Mkuu , hawana ubavu wa kukataa, Donald Trump ndio raisi wa marekani na elon musk ndio.mshirika wake mkubwa, unategemea nini hapo

Pia katika hali ya kawaida utachagua kipi kati ya hivi
Upewe GB 50 kwa Tsh 26,000/- au
26,000/-Tsh upewe GB 9.

Japo najua mafisadi hua hawakosekani kujarib kuwaumiza watanzania kupitia kufanya wizi wa bando na garama kua juu kupita kiasi lakin kwa elon watagonga mwamba.
 
Ndoto za mwendawazimu!
Maisha hayawezi kuwa rahisi jinsi hii!
Jinsi optic fibre ilivyoimbwa sikutarajia hii hali ya mitandao kuwa chini sana itokee.
Star link wao ni nani!!
 
Star link wao ni nani!!
Hapo ni sawa uulize Trump ni nani Wakati unajua kabisa Trump ni dude kubwa ambalo limemfilimba yule Mama hatokaa hasahau Maisha yake yote alianza yule mke wa Clinton akamfilimba akaja huyu Muhindi Mswahili pia akafilimbwa bado unauliza Trump ni nani? Mzee wa kufilimba vimama vinavyotaka kupimana nae uwezo
 
Ndoto za mwendawazimu!
Maisha hayawezi kuwa rahisi jinsi hii!
Jinsi optic fibre ilivyoimbwa sikutarajia hii hali ya mitandao kuwa chini sana itokee.
Star link wao ni nani!!
Mtatukana sana na kuongea shiti sana.
Kiama cha hawa wezi wa bando huku kwetu kimewadia. Mafisadi na cartels waliokua wananufaika kupitia migongo ya watanzania mwisho wao umewadia. Hio sjui mnachukua maoni ni kujarib kupoteza muda tu, watanzania wamechoka kuibiwa. Safari com sasahivi wana adabu na utii.
Unauliza starlink ndio nini ama nani, elewa tu mapinduzi makubwa yanakuja kwenye sekta hii, biashara zinazotumia sana mawasliano ya internet zitaenda kunufaika, makampuni n.k, masuala ya kua kijijini huko huwez kupata internet hadi ufike mjini yamepitwa na wakati, na zaidi ule wizi wa kuwaibia wateja unaelekea kufika mwisho, hao ndio wenye dunia na ndivyo wanavyotaka dunia iwe, sasa wapiga dili mkisikia haya mnaanza kutukana ..tulieni sindano iingie. Welcome to Tanzania Star link.
 
Back
Top Bottom