Stars yawafuata The Cranes

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaondoka nchini leo jioni kuelekea Kampala - Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The Cranes siku ya jumamosi.

Kikosi cha Taifa Stars kinaondoka kikiwa na wachezaji 20, bechi la ufundi 7, pamoja na viongozi kwa shirika la ndege la Rwanda (Rwada Airi) ambapo wanatarajiwa kuwasili uwanja wa Entebe majira ya saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Mchezo wa jumamosi ni wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda, huku mechi hiyo ikichezwa saa 10 jioni katika uwanja wa Nakivubo.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana wake wamefanya mazoezi vizuri katika kipindi chote cha maandalizi, na sasa wako tayari kwa mchezo huo, mipango ikiwa ni kupata ushindi siku ya jumamosi.

Aidha Mkwasa amesema watawakosa wachezaji wawili, Abdi Banda na Mohamed Hussein (Tshabalala) waliopata majeruhi jana wakati wa mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Boko Vatereani, na kusema nafasi zao zitazibwa na wachezaji waliopo kambini.

Wachezaji wanaosafiri ni: Ally Mustafa, Mudathir Khamis, Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Michael Aidani, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla, Saimon Msuva, Deus Kaseke, Ramadhan Singano, Atupele Green, Rashid Mandawa, John Bocco na Ame Ally.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
 
Kila la kheri stars
 
The proposed line up :

Ally Mustafa
S. Kapombe
Haji Mwinyi
Kelvin Yondani
Nadir Harub
Frank Domayo
S. Telela
S. Ndemla
Simon M.
Rashi M.
R. Singano
Sub:
Ame Ally
Deus Kaseke
John Bocco
 
Na wakashinde huko!wakifungwa tu wajue matusi na kuzomewa kuko palepale!tumewachokaaaa!!
 
[TABLE="width: 557"]
[TR]
[TD]Aggr.
[/TD]
[TD="colspan: 2"] Tanzania
[/TD]
[TD]0 - 3
[/TD]
[TD="colspan: 3"]Uganda
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Sat
[/TD]
[TD]20/06/15
[/TD]
[TD]Tanzania
[/TD]
[TD]0 - 3
[/TD]
[TD]Uganda
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Fri
[/TD]
[TD]03/07/15
[/TD]
[TD]Uganda
[/TD]
[TD] -
[/TD]
[TD]Tanzania
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Mechi mbona inaonekana ni tar.03 julai, yaani leo ijumaa, au inakuwaje
 

Game ni kesho Jmos
 
matumizi mabaya ya rasilimali fedha
 
Hawa majamaa wanazingua pamoja na uongozi wao,ingepitishwa sheria ya dharura kwamba wakifungwa au kudraw wananyongwa,utaona watashinda hata magoli kumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…