Startimes kuonyesha kombe la dunia mubasharaa kabisa hapo mwakani

Startimes kuonyesha kombe la dunia mubasharaa kabisa hapo mwakani

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Star.JPG
Kampuni ya StarTimes Tanzania inayouza King’amuzi cha StraTimes, imetangaza kuwa, imepata haki ya kuonyesha michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika mwakani nchini Urusi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Gasper Ngowi, katika hafla ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.

“Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kuwa king’amuzi chetu cha StarTimes kimepata haki za kuonyesha michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika mwakani nchini Urusi, hivyo ni wakati wao sasa kuchangamkia fursa hiyo kwa kulipia ving’amuzi vyao,” alisema Ngowi.

Naye Mkurugenzi na Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luo, amesema: “Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, tumekuja na kitu kipya ambapo tumeongeza chaneli kwenye king’amuzi chetu kwa ajili ya kuwapa burudani zaidi wateja wetu kwani tunawajali sana.”

Pia Luo amesema ili kuwafikia wateja wao kwa haraka na kuwatatulia matatizo yao, katika kitengo chao cha huduma kwa wateja wameongeza watu na kufikia 300 ambapo wateja wao watakuwa wakiwasiliana nao kwa namba 0764700800 na 0677700800.
 
Ngoja nijiandae kununua king'amuzi cha Star Time.
Nimegundua kuwa sina king'amuzi hata kimoja hapa nyumbani.
Sitaki kupitwa na mechi za Kombe la Dunia.
 
Kama litakuwa linaonyeshwa usiku bora kuacha kukinunua hicho king'amuzi ili iwe ticket ya kutoka
 
Hawa jamaa hapana decoder zako ni low quality kwa Picha naona wanataka kuharibu uhondo wa Kombe la Dunia... Tafadharini Wachina kwa kuwa hamtupendi na sisi hatuwapendi.... Cha kwanza waliiharibu TBC kwa kuondosha ile Mitambo ya Sony super quality kwa picture wakaleta matakataka yao yaani kutizama TBC au picha inayotoka kwenye decoder zao bora kutotizama picha mbovu na ukungu ukungu mwingi... Wachina ni zao fake wanacopy mitambo ya wengine kasoro ubora tu... hili ni Tatizo... nadhani tutarejea kwa DSTV tu sasa for sure siwezi tizama mpira kwa decoder za Star times.
 
Hapo umesema mimi nitatafuta decoder ya open view HD ya south Africa
 
Ahsante ! Boresheni na mengineyo nyingi mnajionesha maisha yetu mnaishi nayo.

Biashara na maisha yanakwenda,sio wale wamejikita kwenye biashara wakijifanya maisha yetu hawayajui, kumbe tumekuwa nao.toka enzi zileee
 
Na michuano hiyo itarushwa kupitia channel yako pendwa ya tbc1 [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ngoja nijiandae kununua king'amuzi cha Star Time.
Nimegundua kuwa sina king'amuzi hata kimoja hapa nyumbani.
Sitaki kupitwa na mechi za Kombe la Dunia.
Ununue vingapi tena, wakati wewe ni Marketing officer wa star time
 
Hawa jamaa hapana decoder zako ni low quality kwa Picha naona wanataka kuharibu uhondo wa Kombe la Dunia... Tafadharini Wachina kwa kuwa hamtupendi na sisi hatuwapendi.... Cha kwanza waliiharibu TBC kwa kuondosha ile Mitambo ya Sony super quality kwa picture wakaleta matakataka yao yaani kutizama TBC au picha inayotoka kwenye decoder zao bora kutotizama picha mbovu na ukungu ukungu mwingi... Wachina ni zao fake wanacopy mitambo ya wengine kasoro ubora tu... hili ni Tatizo... nadhani tutarejea kwa DSTV tu sasa for sure siwezi tizama mpira kwa decoder za Star times.
Hilo ni kweli kabisa endapo unatumia decoder zao za zamani. Mimi nilinunua decoder mpya zina quality nzuri tu kwenye picha na kuna channel tatu za sport ni za HD. Kuna siku nilienda kwa ndugu yangu nikamkuta amewasha tv ila muonekano wa picha kwenye channel zilikuwa ovyo sana. Nikabidi niangalie decoder anayotumia nikakuta ni startimes ila niliona ni tofauti na ninachotumia mimi ni decoder za zamani. Mimi Kwakweli sikuwahi kujutia kwa upande wangu hasa ukizingatia ndio channel inayojitahidi kuonesha michuano mingi ya mpira dhidi ya ving'amuzi vingine vya Tanzania (serie A, bundersliga, league ya ufaransa, michuano ya ICC, kufuzuru kwa kombe la dunia kwa bara la ulaya) michuano yote hiyo ni mubashara kabisa.
 
Back
Top Bottom