Startimes, Star Tv sasa waingia kwenye mgogoro wa masilahi

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Dar es Salaam. Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki Kituo cha Televisheni cha Star, imeingia katika mgogoro na Kampuni ya Ving’amuzi ya Startimes na kufikia uamuzi wa kuitoa kurusha matangazo ya televisheni ya kituo hicho.
Hatua hiyo ya Kampuni ya Startimes kuondoa Star Tv kwenye orodha ya vituo vinavyopatikana kwenye king’amuzi chake ilianza juzi.
Startimes ilianza kutoa taarifa kuwa kutokana na matakwa ya Star Tv, wameamua kuitoa kwenye orodha ya chaneli zao bila ya ufafanuzi wa kina kuhusu uamuzi huo.
Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, alipotafutwa kutolea ufafanuzi wa kitendo hicho, alisema hafahamu lolote.
“Sifahamu kwani niko Pemba lakini labda watafute Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (Mkurugenzi wa TCRA) watakuwa wanajua,” alisema Profesa Mbarawa.
Profesa Nkoma hakupatikana jana na juhudi za gazeti hili zilifanikiwa kumpata Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi aliyesema hafahamu sababu za Startimes kuitoa Star Tv katika kurusha matangazo ya dijitali.
“Kulikuwa na matatizo ya makubaliano baina ya pande hizo mbili, Star Tv walilalamika jinsi ya kuonekana kwa chaneli yao kwa mtoa huduma,” alisema Mungi.
Mungi alisema kwa mujibu wa leseni ya kurusha matangazo ya kimataifa, Star Tv inatakiwa kuonekana katika dijitali zote za ndani na uamuzi waliochukua unakiuka makubaliano hayo. “Hata kama kulikuwa na matatizo, hawakutakiwa kuchukua uamuzi huo, kwani wangekutana na mamlaka husika (TCRA) na kusikiliza malalamiko hayo kisha kuwasuluhisha na tatizo hilo likamaliza,” alisema Mungi.

CHANZO: MWANANCHI
 
Purukushani za digitali, anayeumia ni mwananchi/
 
Yani siamini meneja uhusiano wa TCRA anatoa majibu hayo kweli hawana meno hao chezea diallo wa ccm weiwe.
 
Last edited by a moderator:
Hao startimes na startv wakae na kufikia mwafaka, vinginevyo tutaendelea kuumia sisi raia.
 
Ukiona hivi elewa kwamba king'amuzi cha Continental kimedoda sokoni.
 
Ukiona hivi elewa kwamba king'amuzi cha Continental kimedoda sokoni.

Star TV ni mbulula tu kama wamejitoa ili tununue continental kama wameshindwa warudishe leseni watu wanaoweza warushe,itv nao wanataka kujitoa then inabd 2nunue digitek khaaa sebule c itajaa bado deck
 
Last edited by a moderator:
Star TV ni mbulula tu kama wamejitoa ili tununue continental kama wameshindwa warudishe leseni watu wanaoweza warushe,itv nao wanataka kujitoa then inabd 2nunue digitek khaaa sebule c itajaa bado deck
mi nishasema maadamu nilishanunua mapema kabisa king'amuzi changu cha ovyo cha startimes, sitanunua king'amuzi kingine tena iwe continental au digitek! uwezo huo wa kurundika kila king'amuzi kinachoingia sokoni sina! TCRA kwa mtindo hu mtatuua sisi wananchi, tunawalipa ili mfanye kazi gani? napendekeza mfutwe maana sioni umuhimu wa kuwalipa kodi zetu ilihali hakuna mnachokifanya...
 
Kiko wapi tokea amri ya TCRA itolewe juzi mpaka leo STAR TV hawajarejesha matangazo yao kupitia STARTMES. Serikali yenyewe haina meno, huyo TCRA atayatoa wapi, wakati DNA ni ile ile.

Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "nchi yoyote corrupt haiwezi kuwa na mamlaka juu ya wafanyabiashara, na ikifanya hivyo, mfanyabiashara atasema basi kesho siji".
 
Naunga mkono hoja, bora TCRA ifutwe kiundwe chombo kipya chenye meno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…