Startimes wanadai tulipie Local channels

Startimes wanadai tulipie Local channels

mnono

Member
Joined
Jun 27, 2016
Posts
37
Reaction score
19
Week mbili zilizopita watoa huduma wa Startimes walinipigia na kuniuliza kwanini nimekaa muda mrefu bila kulipia king'amuzi nikawajibu watoto wakuangalia katuni hakuna hivyo sihitaji hizo channel za kulipia. Wakasema wanafanya upgrading ya software hivyo nisipolipia sitaweza kuona, kuanzia weekend hii signal imeanza kufumbua, napata ujumbe no service, no signal kwa local channels, lakini channel zao za matangazo zinaonekana. Jana umekua unatokea ujumbe this bundle belongs to local channels recharge to continue watching.

Tafadhali naomba ufafanuzi kwa wahusika hivi siku hizi tunalipia local channels? Nakumbuka tuliambiwa na TCRA local channes ni bure, kama kuna mabadiliko tunaomba Startimes watujulishe local Channels tunalipia kila baada ya miezi mingapi? TCRA na Wizara ya habari tunaomba ufafanuzi, kwani kinachotokea ni kero sana.
 
Unatumia king'amuzi gani mkuu? Dish au Antenna? Mimi natumia cha Antenna toleo la kwanza kina miaka kama minne sijalipia hadi jana usiku kilikuwa kinapiga kazi kwa local channels na hawajawahi nipigia simu.

StarTimes Tanzania njooni mtoe maelezo huku.
 
hahhaha siku hizi njaa kali hadi mchina kakupigia simu!
 
Back
Top Bottom