State officials banned from traveling abroad without Uhuru's permission

G4rpolitics

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
4,369
Reaction score
5,248
Kama huku kwetu, Kenyatta naye kaanza bana matumizi kwa watumishi wote wa umma, habari ipo hapa...

Photo: Boniface Okendo, Standard

Kenya's government officials have been banned from travelling outside the country unless they have express permission from President Uhuru Kenyatta.

"This is to notify you that it has been decided, until further advised otherwise, no government official will travel outside the country without clearance by the president," read a circular by Chief of Staff and Head of Public Service Joseph Kinyua to Cabinet Secretaries. the Attorney General and Principal Secretaries.

"For avoidance of doubt, the officials in reference include Cabinet Secretaries, Principal Secretaries and Officers in Ministries, Chief Executive Officers of Parastatals and their officers, and Board of Directors of Parastatals.

The letter dated September 13 was copied to the Ministry of Interior and Coordination of National Government as well as the Ministry of Foreign Affairs.

Kinyua said the directive takes effect immediately, without indicating the reason for the drastic order.

In the recent past, some individuals have been stopped by Immigration from boarding their flights as officials at the airport demanded clearance letters.

Human rights activist Maina Kiai was in August temporarily held at Jomo Kenyatta International Airport for failure to provide prove of clearance. He was later allowed to proceed with his trip after intervention from Director of Immigration

In the same month, shortly after the General Election, Independent Electoral and Boundaries Commission’s Roselyne Akombe missed her flight to the US as airport officials demanded to see her travel clearance. She was later allowed to travel after a night long delay.




source Standard online
 
Ila ubahiri cyo mzuri,unabana matumizi ili iweje ...Hasara zake ni nyingi kuliko faida
 
Magufuli mengi anayofanya ni faida ,sema sisi tumekuwa na siasa nyingi kupita kiasi. Ndio maana hata wakenya wafuasi wa uhuru wanamchukia magufuli sio kwa sababu ana ugomvi nae lakini wanaona magufuli kusema ukweli kamshinda mbali uhuru kiutendaji hivyo wanakuwa wanatamani uhuru afanye kama magufuli , unakuta hao wafuasi wake wanasema kimya kimya he need to be like magufuli.
 
Hili ni jambo zuri sana kwa viongozi wa EA kujaribu kujifunza yale mazuri yanayofanyika kwa jirani yako, ni ukweli usiopingika kwamba, ukiondoa ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza, Magufuli ni rais wa kuigwa sio tu na wakenya, bali Afrika nw dunia nzima. Mimi ninakumbuka hili ni jambo la tatu kwa Kenya kujifunza na kufuata nyayo za Magufuli, kwanza ni kuamua kwamba pesa zote za serikali zisiwekwe tena katika mabenki ya biashara, pili ni kwa magavana wapya kuwasimamisha na kuwaachisha kazi wafanyakazi wengi toka county mbalimbali waliotuhumiwa na rushwa ili kupisha upelelezi, na hili la kuzuia safari za nje hadi kibali cha rais, na bado Kenya kuna mambo mengi mazuri ya kujifunza toka Tanzania chini ya utawala wa Magufuli.
 
Tunategemea yeye Uhuru Kenyatta ataongoza katika kupunguza safari za nje, amekua ni mfano mbaya katika kipindi chake kilichopita kwa kufanya safari nyingi za nje tena akitumia ndege ya rais akiambatana na jopo la watu wengi, ni ukweli usiopingika kwamba Uhuru Kenyatta na serikali yake imepoteza pesa nyingi sana za serikali ambazo zingeweza kuokolewa kama angekuwa makini japo nusu ya Magufuli.
 
Nawaza tu kwa kutumia vidole!

Pamoja na uzuri wa suala hili lakini kwa nini ije wakati huu wa uchaguzi? Labda kuna mambo mawili au matatu!


Mosi, Kutokana na serikali ya Uhuru kupigiwa kelele kwa matumizi mabaya ya rasilimali kipindi cha kuelekea uchaguzi uliofutwa, sasa anajaribu kurejesha imani kwa wakenya kuwa serikali yake itakuwa ni kama sio ya kubana matumizi, basi ni ya kutumia vizuri rasilimali za nchi! Hii anahisi inaweza kumjengea imani kwa wakenya ili wamchague tena kwa mara nyingine!


Pili, Ni ukweli usiopingika kuwa uchaguzi wa kenya kama zilivyo chaguzi nyingi unatumia sana pesa! Na kenya haikutegemea kuwa kutakuwa na uchaguzi wa marudio, na pengine bajeti hiyo haikuwepo kabisa! Huenda hii ikawa pia ni njia ya kuhakikisha serikali inapata fedha zote bila kuathiri sana uchumi wa nchi ambao unaporomoka! Hakuna asiyejua matumizi ya hawa viongozi wa serikali wanapokuwa wanaenda ughaibuni!


Tatu, kwa namna moja ama nyingine, kitendo hiki kinaweza kuwa ni njia ya kuonyesha kuwa, kama ilivyo katiba ya kenya, uhuru ndiye rais halali wa kenya kwa sasa hadi hapo mwingine atakapoapishwa! Ikumbukwe kumekuwa na malalamiko kutoka nasa kuwa Uhuru hakupaswa kuzindua Bunge kwani sio rais halali, sasa kuonyesha meno yake anaamua kufanya kitu kwenye serikali yake ambacho kitawaumiza viongozi wa serikali lakini kitamjengea heshima kwa wananchi!
 
Issue hapa sio kubana matumizi uchaguzi wa marudio.
 
Pesa za IEBC lazma zitoke Mahali, Lakini anavyofanya Uhuru itabidi nitumie ule msemo wa 'Usipo ziba nyufa....Utajenga ukuta'


Ni kazi bure anachojaribu kufanya, Uchaguzi Mpya unahitaji 15 Billion cash ($150 Million) kile ambacho ameagiza kifanyike eti trip za nje hazitafikisha hizo pesa....

Kama anataka pesa kweli, inasemskana zaidi ya $1Billion mali ya uma hupotea kwa rushwa, angeambia tume ya rushwa nimekupa mamlaka na nitakulinda, fwata yeyote alieiba pesa na uziregeshe angepata zaidi ya 15 billion ksh
 
Mimi ninaehani tamko hili halilengi kupata pesa kww ajili ya uchaguzi wa marudia, kwa sababu ndani ya muda wa mwezi mmoja uliobaki hakutakuwa na safari nyingi za kiserikali, tamko hili limetolewa ili kutoa dira ya uongozi wake utakavyokuwa kama akichaguliwa tena, kumbuka alipigiwa kelele nyingi sana juu ya tabia yake ya kupenda kusafiri akilinganishwa na Kibaki na Magufuli, kumbuka Kagame alikuwa rais wa kwanza kusema hadharani kwamba anaunga mkono juhudi za Magufuli za kuzuia safari za viongozi hadi kwa kibali cha rais, Uhuru anakuwa rais wa pili kufuata staili hiyo ya uongozi, hata kama Raila atachaguliwa ninauhakika atafanya hivyohivyo, kwa sababu safari za nje zilitumika kuiba fedha nyingi za serikali.
 
Uchaguzi mpya ndo umesababisha serekali kuchukua hatua hii mkuu, pia ukame umetumia pesa zote za "emergency fund" sasa inabidi tu tumie pesa ambazo zilikua zimepangiwa miradi miengine. Ni kweli pesa zitakazo 'okolewa' ndani ya maezi michache haitafikisha.. Si eti serekali haina pesa, ni kwamba pesa ziko lakini tayari zilikua zimeshapigiwa mahesabu ya vitu vyengine, sasa hizo billioni 15 ksh zitakazo tumika kwa uchaguzi, kuna mahali ndani ya bajeti ya kawaida kutakua na pengo, hivyo basi serikali imeamua kutafuta njia mbadala kujaza hilo pengo....

Tangu mwezi wa Feb hadi Oct Ukame ulikua umezidi , pesa nyingi zilitumika nje ya bajeti Government declares drought a national disaster – Presidency


Government officials will be denied foreign and local trips, furniture, vehicles and hospitality treatment to fund repeat election and food relief to counter continued drought. Treasury Cabinet Secretary Henry Rotich says the polls may cost upwards of Sh15 billion and will need the State to tighten its belt to finance it. ALSO READ: Orengo’s new order to IEBC ahead of repeat presidential election The Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) had submitted plans to spend only Sh12.2 billion but the CS says security expenses will increase the figure by over Sh3 billion. “To finance some of those emerging priorities, we have to restructure some expenditure and we are targeting non-essential expenditure particularly travel, both domestic and foreign. Foreign is actually banned for now so that we can allow resources available to be directed to conduct another election,” he said. “We are also reviewing hospitality training and non-priority development expenditure,” he added. Kenya’s budget shortfall has always been a thorn in the flesh, with Treasury anticipating a Sh524.6 billion hole in this financial year’s Sh2.29 trillion budget. Expensive affair The surprise repeat election is a setback, especially since Kenyan elections remain an expensive affair with the National Treasury having spent Sh60 billion from the exchequer to ensure success of the August 8 poll. The money was split between IEBC, security forces as well as the Registrar of Political Parties and the Judiciary. Police got Sh1.6 billion of food rations and Sh4 billion of allowances as well as Sh3.8 billion for enhanced security operations in Lamu, Mandera, Wajir and other hotspots but are requesting an additional Sh8.2 billion.
Read more at: Government officials denied foreign trips, vehicles and hospitality treatment

 
Atawaambaiaje tume ya rushwa wakamate wala rushwa akati na yeye familia yake inatuhumiwa kujinyakulia ardhi kubwa hapo kenya?
 
Is this a Total Ban or just to let the election pass?
 
Kuna mwenzangu ameuliza hapo juu na mimi ninauliza, je baada ya uchaguzi watarudisha haya yaliyozuiliwa au ndiyo vitaendelea moja kwa moja kwa maoni yako?, Pili ninakumbuka kuna mwenzenu mmoja hapa hapa alikua akibishana sana baada ya kuambiwa kwamba uchaguzi wa marudio utazidi kuumiza mapato ya Kenya, yeye alitetea kwa kusema kwamba, kwa sababu kipengele cha kurudia uchaguzi kipo kwenye katiba ya Kenya, kwahiyo bajeti ya serikali iliyopita sio tu iliweka pesa ya uchaguzi, bali pia ilishatenga ya uchaguzi wa marudio endepo utatokea, sasa leo unasema serikali inabidi itafute pesa ya uchaguzi wa marudio, mbona mnakanganyana?
 
Kwa maoni yangu, baada ya uchaguzi bado watazulia zulia kidogo hadi waregeshe zile pesa walizotumia kwa marejeo ya uchaguzi alafu baada ya kama miezi mitatu hadi sits, mambo yatarusi vile... Kumbuka hata hii ban Ambayo Rais ameweka, ni kwa mkono mmoja wa serekali tu (executive), Kisheria rais hana mamlaka ya kuzulia bodi yoyote nje ya 'executive' bado majaji na wabunge na 'independent commisions' kama vile iebc,Kenya human rights commision, Indepent police oversite na commision zengine wanaweza safiri...


Alafu, kuhusu kipengeke cha katiba kuongelea uchaguzi, kama tungekua nchi tajiri hizo pesa zingekua zimetengwa kando kitambo sana, lakini vile ilivyo kenya kuna system flani wizara ya afya ... Anyway. Kwa kigupi ntakwambia hivi... Uchaguzi wa kwanza ulitrngewa bajeti ya $600Million (60 Billion ksh) sasa uchaguzi huo ulifutwa, uchaguzi h mwengine mpya wanadai $150Million, wafanyikazi wamuhimu wanaohitajika ni wale wale, mshahara ule ule, tofauti nkwamba watachapisha makaratasi ya rais pekew.... lazma kuna pesa nyengine zinatoka kwa ile $600m
 
Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, inawezekana ama wakenya mlio wengi humu ndani hamuijui vizuri katiba yenu, au katiba yenyewe ndiyo mbaya. Rais wa nchi amepewa jukumu la kusimamia na kuendeleza uchumi wa nchi, serikali ndiyo yenye jukumu la kusimamia ukusanyaji na usimamiaji matumizi bora ya mapato ya nchi, sasa inawezekanaje serikali ikiongozwa na rais iwe na jukumu la kukusanya na kubuni vyanzo vya mapato lakini isiwe na uwezo wa kusimamia matumizi yake.

Kwa mfano umesema hapo juu kwanza udhibiti huo hautowagusa wabunge na wafanyakazi wa mahakama, wao watatumia pesa kadri apendavyo sasa hili limekaaje?, Pili katika andiko ulilonitumia hapo juu, linasomeka kwamba serikali imeamua kufuta shughuli na safari zisizokua na umuhimu sana, ili kukusanya pesa za uchaguzi, ila uchaguzi ukipita na pesa zikisharudi, watarudisha hizo shughuli zisizokua za lazima ili ziendelee kutafuna pesa, je unataka kuniambia baada ya uchaguzi hakuna mambo mengine muhimu zaidi zinazoweza kufaidika na hizo peza, kwanini mzirudishe tena kwenye safari za viongozi, semina na kununua furniture za viongozi, tena wanaagiza toka nje ya nchi?
 
Reactions: Oii
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…