State Oil yakubali kuilipa Equity Bank Tsh. Bilioni 47 za Mkopo uliokuwa unabishaniwa

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Hatimaye Kampuni ya State Oil Tanzania Limited imekubali yaishe mahakamani kuhusu malipo ya mkopo wa Dola 18.64 milioni za Marekani (Sh47 bilioni) za Benki za Equity, Equity Bank Tanzania Limited (EBT) na Equity Bank Kenya (EBK) uliokuwa unabishaniwa.

Hii inatokana na uamuzi wa kampuni hiyo kuiondoa mahakamani kesi iliyokuwa imeifungua ikipinga malipo ya mkopo huo kwa madai haikuwahi kukopeshwa na benki hizo, badala yake imekubali kuzilipa benki hizo Dola 13.5 milioni za Marekani (Sh35 bilioni).

Kampuni hiyo awali ilifungua kesi Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam dhidi ya benki hizo ikipinga kudaiwa fedha yoyote na benki hizo.

Hata hivyo, benki hizo pia zilifungua madai kinzani zikidai kuwa zinaidai kampuni hiyo Dola 26.47 milioni za Marekani likiwa ni deni la mkopo ambao ziliipatia kampuni hiyo Novemba 21, 2018.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake ilikubaliana na madai ya kampuni hiyo na kuipa ushindi ikieleza benki hizo hazikuwahi kuikopesha kiasi hicho cha fedha.

Benki hizo zilikata rufaa Mahakama ya Rufani zikipinga hukumu hiyo ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake ilioutoa Mei 16, 2024 ilibatilisha hukumu hiyo ya Mahakama bila hata kusikiliza hoja za msingi za rufaa ya benki hizo.

MWANANCHI
 
Chupuchupu equity bank waachiwe manyoya
 
Kuna uzi aliandika MMM X kuhusu hii michezo ya wahuni kukopa mabenk mizigo mirefu halafu wanala nyoya.

Kuna benk zimekopa hadi B150 na mkopwaji akashinda mahakamani asilipe.
 
Hatimaye Kampuni ya State Oil Tanzania Limited imekubali yaishe mahakamani kuhusu malipo ya mkopo wa Dola 18.64 milioni za Marekani (Sh47 bilioni) za Benki za Equity, Equity Bank Tanzania Limited (EBT) na Equity Bank Kenya (EBK) uliokuwa unabishaniwa.

Hii inatokana na uamuzi wa kampuni hiyo kuiondoa mahakamani kesi iliyokuwa imeifungua ikipinga malipo ya mkopo huo kwa madai haikuwahi kukopeshwa na benki hizo, badala yake imekubali kuzilipa benki hizo Dola 13.5 milioni za Marekani (Sh35 bilioni).

Kampuni hiyo awali ilifungua kesi Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam dhidi ya benki hizo ikipinga kudaiwa fedha yoyote na benki hizo.

Hata hivyo, benki hizo pia zilifungua madai kinzani zikidai kuwa zinaidai kampuni hiyo Dola 26.47 milioni za Marekani likiwa ni deni la mkopo ambao ziliipatia kampuni hiyo Novemba 21, 2018.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake ilikubaliana na madai ya kampuni hiyo na kuipa ushindi ikieleza benki hizo hazikuwahi kuikopesha kiasi hicho cha fedha.

Benki hizo zilikata rufaa Mahakama ya Rufani zikipinga hukumu hiyo ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake ilioutoa Mei 16, 2024 ilibatilisha hukumu hiyo ya Mahakama bila hata kusikiliza hoja za msingi za rufaa ya benki hizo.

MWANANCHI

Yule lawyer aliyesaidia huu ujinga anaendeleaje? Bwana Frank?
 
Back
Top Bottom