Asante sana mkuu, nitayafanyia kazi mawazo yako, asante sana kwa mchango wako.
Vipi upo kwenye hii biashara na ungeweza kumshauri nini muanzaje na je unadhani start up capital inayohitajika ni kiasi gani kwa wastani?
Na je kama ukiajili mfanyakazi mshahara unatakiwa uwe kiasi gani?..
Mkuu sipo kwenye biashara hii kwa sasa ila nilishawahi kuifanya kwa kipindi fulani huko mikoani. Katika
Business Plan zangu, huwa ninaweka
exit stratergy, hivyo baada ya kupata kile nilichokitaka ktk biashara hii someone else took over. Na kwa sasa biashara imekuwa sana, lakini nikikusimulia namna ilivyoanza, unaweza usiamin (
its very motivational).
Kwa uzoefu wangu, (
huku Site) biashara hii unaweza ukaianza na mtaji mdogo (
3m to 4m) na bado ukafanikiwa (
lakin ni kama matumizi yako hayatazidi mapato yako). Wengi walianza na mitaji midogo, halafu wakawa wanawekeza ile faida inayotengenezwa kama mtaji. Kwa hiyo nikutoe wasiwasi na huo mtaji wako wa 15M. Challenge kubwa kwa hapa Dar ni
RENT na mahali muafaka pa kufanyia hiyo biashara
Pia ninakushauri ufanye kitu inaitwa
DEBT FINANCING, itakusaidia sana kwenye masuala ya kodi huko TRA. (
Geuza huo mtaji wa 15m kama mkopo kutoka kwenye familia au rafiki). Hii itakulazimu kufanya deductions (
principal + interest) kwenye mapato yako. Hivyo itakupunguza
taxable income kwa kipindi cha marejesho. Kama utahitaji
Tax Planning Measures zaidi (
for tax saving purposes tena legally) unaweza ukaniPM
Kuhusu namna ya kulipa mshahara
Hili suala (
kwa biashara hizi) kila mtu huwa analiangalia anavyoliona kulingana na ukubwa wa biashara pamoja na mapato yake kwa mwezi, bila kusahau ujuzi wa mfanyakazi husika. Personally, huwa napenda kutumia "
performance indicators" kama njia ya kumlipa mfanyakazi, lakini huwa silipi chini ya Minimum wage ya serikali. Na allowance kama ya nauli na chakula (
akiwa kazini) ni muhimu kama sivyo elewa kuwa atachukua mwenyewe kwa njia nyingine
N:B
Compliance ni muhimu sana, hivyo nakushauri usajili biashara yako katika mamlaka zinazohusika (itakusaidia kwenye mambo ya kibenki, utaepuka usumbufu na utajenga image nzuri kwenye jamii. Na kubwa zaidi utashiriki katika ujenzi wa Taifa lako kupitia Kodi yako.
Mamlaka zinazohusika ni BRELA, TRA na Local Government Authorities (
kwa case yako ni Manispaa ya Kinondoni)