Nina Crown athletic ya mwaka 2006. Hivi karibuni nimebadilisha steering rack yote pamoja na mkanda wa steering baada ya ile ya kwanza kukatika.
Baada ya kubadilisha na kuweka nyingine Steering imekuwa ngumu sana haswa wakati wa kureverse na na wakati wa kukata kona.
Cha ajabu gari ikiwa kwenye mwendo wa kasi ni kwamba steering inarudi kuwa lain kama kawaida yake.
Naomba kueleweshwa kutoka kwa wataalam wa hizi power steering nini kinasababisha tatizo hili la steering kuwa ngumu?