Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ameonesha masikitiko yake bungeni baada ya kuuliza swali mara tano kuhusu changamoto ya upungufu wa wodi katika Kituo cha Afya Kiyagara, bila serikali kuchukua hatua.
Mbunge huyo ameuliza swali hilo tarehe 28 Januari 2025, katika Mkutano wa 18, Kikao cha Kwanza Bungeni Jijini Dodoma. Ameeleza kuwa hali katika kituo hicho ni mbaya, ambapo wagonjwa watano wanalazimika kulala katika kitanda kimoja, hali inayohatarisha afya na ustawi wa wagonjwa.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainabu Katimba, amemhakikishia Mbunge huyo kuwa serikali itaendelea kupeleka fedha ili kutatua changamoto za sekta ya afya katika jimbo hilo.
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, ametoa agizo kwa Naibu Waziri huyo kuhakikisha kuwa serikali inakuja na majibu mahsusi juu ya suala hilo.