KERO Stendi Kuu ya Mabasi Dodoma inalazimisha abiria kulipa ushuru Tsh. 300 hata kama una tiketi ya basi mkononi

KERO Stendi Kuu ya Mabasi Dodoma inalazimisha abiria kulipa ushuru Tsh. 300 hata kama una tiketi ya basi mkononi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha kero yangu ambayo imekuwa ya muda mrefu katika stendi kuu ya mabasi Dodoma ambapo wasafiri wanaoingia humo hulazimishwa kulipa ushuru wa halmashauri kiasi cha tshs 300/= hata kama tayari ana tiketi ya basi mkononi.

Hii ni tofauti na stendi kuu za mikoa mingine ambazo kama unakuwa na tiketi unaruhusiwa kuingia kwa vile tayari ushuru unakuwa umelipwa na basi unalosafiri nalo.

Soma Pia: Watoza ushuru stendi ya mabasi Magufuli hawatoi risiti hivyo kuikosesha mapato manispaa

Sasa watu tunajiuliza kwamba Dodoma kuna nini?
 
Hii si sawa kabisa, nachojua unapokuwa na tiketi unapita bila kulipa ushuru wa kuingia.
 
Ulivyowaambia kwamba hio sio sawa na ticket unayo walijibu nini ? na kama hauna hio mia tatu ina maana utaacha kusafiri ? Huyo jamaa hana wakuu wake wa kazi upeleke hio kero na kwao huenda ni huyo samaki mmoja ndio ameoza anafanya wote waoze (hivyo anapaswa kufukuzwa kazi)
 
Siyo peke yako,hata mimi nilishalazikishwa kutoa ushuru wakati nina tiketi.Haijukikani kama ni tozo ya Jiji au wahuni wachache wa pale stendi.Ni bahati mbaya tumashindwa kulalamika,maana mara nyingi huwa inatukuta abiria ambao tuna haraka ya kuwahi mabasi
 
Ndo shida ya miji yenye mizunguuko midogo ya hela yaani wanakaba Kila kona kwa kulazimisha, wakati stand zingine kama Nyegezi unaonyesha tu message Kwa simu tena wakati mwingine unaemsindikiza anakutumia ticket yake na unaonyesha unakatiza tu (wizi sio mzuri msifanye hivi)
 
Naomba kuwasilisha kero yangu ambayo imekuwa ya muda mrefu katika stendi kuu ya mabasi Dodoma ambapo wasafiri wanaoingia humo hulazimishwa kulipa ushuru wa halmashauri kiasi cha tshs 300/= hata kama tayari ana tiketi ya basi mkononi.

Hii ni tofauti na stendi kuu za mikoa mingine ambazo kama unakuwa na tiketi unaruhusiwa kuingia kwa vile tayari ushuru unakuwa umelipwa na basi unalosafiri nalo.

Soma Pia: Watoza ushuru stendi ya mabasi Magufuli hawatoi risiti hivyo kuikosesha mapato manispaa

Sasa watu tunajiuliza kwamba Dodoma kuna nini?
ichi kitu mimi ndio kinanikera nikienda Dodoma. halafu, wanakuwa na karatasi nyingi mkononi, inawezekana zingine hata hazifiki jiji, wanakula wale vijana.
 
Back
Top Bottom