KERO Stendi ya Mabasi na Daladala ya Nanenane - Mbeya ina mashimo, mamlaka zisisubiri mgomo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Stendi ya Mabasi na Daladala ya Nanenane iliyopo Mbeya imekuwa na barabara zenye ubora mdogo kutokana na uwepo wa mashimo mengi ambayo yamekuwa yakisababisha usumbufu kwa Watumiaji iwe wa Vyombo vya Moto au wanaotembea kwa Miguu.

Tunachojiuliza ni kuwa Mamlaka husika zinasubiri migomo ya wenye vyombo vya Moto ndio hatua zianze kuchukuliwa? Kwanini mamlaka husika hazichukui hatua na pesa za ushuru zinakusanywa kila siku?

Viongozi wanaohusika wanatakiwa kuwajibika, hii ni aibu ya Mkoa.

 
Boda boda wamchangia Tulia Ackson hela ya fomu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…