Ni shidaDaaah! Hii nchi bhana, katika pitapita zangu nimeibukia maeneo ya Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.
Halmashauri ya Wilaya hiyo imefanikiwa kujenga Stendi mpya ya mabasi eneo la Forest lakini kinachoendelea hapo hakina afya sana kwa watumiaji, kwani miundombinu mingi ni mibovu.
Kulikuwa na haja gani ya kuanza kutumia Stendi ya Mabasi ya Forest Mlowo (Songwe) kabla haijakamilika?
Nilipoulizia nimejulishwa kuwa Stendi hiyo ilianza kutumika hata kabla ya kukamilika vizuri, najiuliza hivi kulikuwa na ulazima gani wa kuharakisha magari kuanza kupita hapo kabla ya maboresho kukamilika?
Na wasivyokuwa na aibu Watu wa Halmashauri wanakusanya ushuru lakini ukiangalia mambo mengi bado hali ni tete ikiwemo fremu kuwa ndogo, majani ni mengi ndani ya Stendi na hata njia yenyewe ya ndani ina mashimo kadhaa.
Embu rekebisheni stendi kwanza ndiyo muendelee kukusanya huo ushuru wenu.
Tunakumbushana tu miundombinu Bora ni muhimu kwa sisi Wananchi kuliko huo ushuru wenu ambao mnakusanya na kujaza matumbo yenu.
CCM ni janga kila mahali👿Daaah! Hii nchi bhana, katika pitapita zangu nimeibukia maeneo ya Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.

Hii wapi mkuu?